
Wananchi wametakiwa kujitokeza kushiriki kwenye mchakato wa uchaguzi mkuu kwani ni njia ya msingi ya kuhakikisha sauti zao zinasikika,na kuchagua viongozi wanaowapenda na wenye uwezo wa kuleta maendeleo na kutatua changamoto zilizopo katika jamii.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa NaCoNGO mkoa Morogoro na Mkurugenzi wa Tanzania Initiative for social and Economic Relief (TISER)Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tanzania Iniative for Social and Economc Relief (TISER),Otanamusu Nicholas wakati akiongea na waandishi wa habari mjini Morogoro.
“Wananchi wote tunapaswa kutumia haki yetu ya kidemokrasia kwa kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025”,ameeleza.
Nicholas amesema nchi yetu ya Tanzania ina amani na upendo wa kutosha,na hivyo katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu wanapenda kuona amani inaendelea kuwepo na kuwapa nafasi kila mwenye haki ya kupiga kura kushiriki katika zoezi hilo.
“Kupiga kura ni haki ya kikatiba ya kila raia,kushiriki uchaguzi ni njia ya kutekeleza wajibu wa uraia na kuhakikisha sauti ya wananchi inasikika katika kuleta maendeleo”,amesema Nicholas.
Amesema viongozi watakaochaguliwa ndio watakuwa chachu ya kuleta maendeleo ndnai ya nchi katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu,kilimo na maji,hvyo kila mwananchi atambua kura yake ni muhimu sana na kujitokeza kwa wingi katika mchakato huo.
"Katika kipindi cha mchakato mzima wa uchaguzi tuepuke kauli za chuki,lugha mbaya,ambazo tunajua zinaweza kuleta sintofahamu kwa upande mmoja au mwingine na kusababisha vurugu za hapa na pale", amesema.
“Niwaombe wanasiasa,wagombea,tuepuke kauli za chuki,tunaponadi sera zetu jukwani tutumie lugha nzuri ambazo zitafanya sera zako kueleweka na kukubalika ndani ya jamii”,amesema.

By Mpekuzi
Post a Comment