DIWANI NDOLELEJI AELEZEA MIKAKATI YA UTEKELEZAJI MIRADI KWENYE KATA HIYO |Shamteeblog.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Ndoleleji, Mhe. Josephat Limbe akizungumza kwenye mkutano wake wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Ndoleleji, ukiwa na lengo la kuwapa wananchi majibu kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Kata hiyo Oktoba 6, 2026

Na Sumai Salum-Kishapu


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Ndoleleji, Mhe. Josephat Limbe, amesema mradi wa maji unaotekelezwa katika Kijiji cha Ndoleleji utakamilika ndani ya siku 13 kuanzia Oktoba 6, 2026 na kunufaisha wananchi wa Kijiji cha Ndoleleji pamoja na Shokashoka.


Limbe ameyasema hayo kwenye mkutano wake wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Ndoleleji, ukiwa na lengo la kuwapa wananchi majibu kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Kata hiyo. Amesema kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kuondoa changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wa maeneo hayo.


Katika hatua nyingine, Limbe amesema Halmashauri tayari imekitengea bajeti Kijiji cha Shokashoka kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa shule shikizi, huku akieleza kuwa Serikali kupitia Halmashauri inaendelea na mpango wa kuboresha miundombinu na mazingira wezeshi kwa wananchi, ikiwemo kuunganisha umeme katika vitongoji vya Mwasheli, Nyaguganwa na Shokashoka.


Limbe pia amesema Kijiji cha Ndoleleji ni miongoni mwa maeneo yatakayojengewa kituo cha afya kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri, hatua inayolenga kusogeza huduma za afya karibu na wananchi. Aidha, amesema kipande cha barabara kinachounganisha Idisa na Ndoleleji ambacho kimekatika mawasiliano kinatarajiwa kufanyiwa matengenezo ndani ya mwezi mmoja, kupitia mpango wa dharura wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), hasa kuelekea kipindi cha mvua.


Limbe pia amewahimiza wanawake, vijana na watu wenye mahitaji maalumu kuendelea kujiorodhesha kwenye vikundi vinavyokidhi vigezo ili kunufaika na mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri. Amesema Halmashauri imetenga Shilingi milioni 500 kwa ajili ya kuwezesha vikundi vilivyokidhi sifa za kukopesheka katika mwaka uliopita, huku akiwataka kutumia fedha hizo kuanzisha miradi yenye tija na kuimarisha uchumi wa kaya. Aidha, amewataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya athari za mvua za El Niño, ikiwemo kuhifadhi chakula cha kutosha.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Ndoleleji, Mhe. Josephat Limbe akizungumza kwenye mkutano wake wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Ndoleleji, ukiwa na lengo la kuwapa wananchi majibu kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Kata hiyo Oktoba 6, 2026


Akizungumzia mradi huo , Msimamizi wa mradi kutoka kampuni ya Mponela Constraction Ltd. Mhandisi. Juma Masanja amesema hatua mbalimbali za ujenzi zinaendelea na kukamilika kwake kutaiwezesha huduma ya maji kuwafikia wananchi waliokusudiwa katika Kijiji cha Ndoleleji na kitongoji cha Shokashoka.


Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilayani humo, Shija Ntelezu, amesema chama hicho kitaendelea kushirikiana na viongozi wa Serikali na wananchi katika kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kama ilivyo ahadi ya ilani ya Chama hicho huku akisisitiza umuhimu wa wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli zinazolenga kuboresha maisha yao.


Baadhi ya Wananchi waliohudhuria mkutano huo, Julius Msoma na James Luges wamepongeza hatua ya viongozi kusikiliza kero zao na kutoa majibu kuhusu miradi ya maendeleo, huku wakisisitiza umuhimu wa kukamilishwa kwa wakati kwa mradi wa maji na miundombinu mingine inayohitajika katika maeneo yao.

Msimamizi wa mradi kutoka kampuni ya Mponela Constraction Ltd. Mhandisi. Juma Masanja
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilayani humo, Shija Ntelezu
Diwani wa Viti maalumu Tarafa ya Kishapu wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Marry Chenge
Mwenyekiti wa Kijiji cha Ndoleleji wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Pius Pawa Nyandi

























































By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post