Polisi wa eneo la Navakholo Kakamega nchini Kenya wamemkamata mwanaume anayetuhumiwa kumuua mkewe kutokana na ugomvi unaohusu ugali.
Bwana huyo aliyefahamika kwa jina la Joseph Boyi, mwenye umri wa miaka 44 kutoka kijiji cha Emakuya anadaiwa kumuua mkewe Florence Nakonjio usiku wa manane baada ya kurudi nyumbani akiwa amelewa, alianza kudai chakula cha jioni licha ya kuwa alikuwa amepewa chakula cha jioni kabla ya kwenda kunywa.
Mtoto wa bwana huyo alianza kusikia ugomvi wa wazazi wake na akasikia mama yake akilalamika kuwa baba yake anataka kumuua, na baada ya kumuuliza baba yake kwa nini anafanya hivyo pia alitishia kumpiga.
Mkuu wa eneo la Navakholo Bw. Titus Muganda amesema mtuhumiwa amekamatwa na jembe alilotumia kumuua mke huyo pia limepatikana. Kwasasa mtuhumiwa anashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Kakamega hadi atakapofikishwa Mahakamani.
By Mpekuzi
Post a Comment