Polisi nchini Kenya wanamshikilia msichana wa miaka 15 baada ya kudaiwa kumchoma kisu mpenzi wake wa miaka 19 hadi kufa katika eneo la Lang’ata jijini Nairobi.
Majirani wanasema wawili hao waliokuwa na ugomvi, na msichana aliishia kumchoma kisu mwanafunzi huyo wa kidato cha pili mara mbili kifuani. Mama wa mtoto huyo mwenye umri wa miaka 15 hakubali kuwa binti yake wa Darasa la Sita anaweza kufanya mauaji hayo.
Majirani wanasema walisikia mayowe kutoka nyumbani na wakakimbilia kuangalia nini kinaendelea, na kumkuta marehemu akilalamika kwa maumivu makali huku akitokwa damu na baadaye alikimbizwa hospitali ambako alifariki.
Mashuhuda wanasema msichana huyo ambaye kwa kawaida yake huwa na mvulana huyo majira ya mchana, ilikwenda kwa mpenzi wake na walikuwa wakizozana kuhusu tuhuma kwamba mvulana huyo ana msichana mwingine.
By Mpekuzi
Post a Comment