Botswana imeingia kwenye orodha ya nchi za Afrika zilizotanganza kuwa zitaanza kufundisha lugha ya Kiswahili katika shule zake.
Waziri wa Elimu ya Msingi wa Botswana Bw. Fidelis Molao, amesema Kiswahili kitaanza kufundishwa hivi karibuni na wanataka watoto na raia wa nchi hiyo wakifahamu Kiswahili ambacho kinaendelea kukua kwa kasi.
Nchi zilizopo kwenye eneo la Maziwa Makuu zinaendelea kuwa na ushawishi mkubwa wa kiuchumi na Botswana inaona wananchi wake kufahamu lugha hiyo kutahimiza ushirikiano.
Mpango huo wa kufundhisha Kiswahili unaonekana kufuata mkondo wa Afrika Kusini ambako Kiswahili kinafundishwa kama lugha ya ziada baada ya Kiingereza na Kiafrikana.
Kiswahili pia kinafundishwa katika nchi nyingine dunia ikiwa ni pamoja na Ujerumani, Uingereza, Canada, Russia, China, Australia na India.
By Mpekuzi
Post a Comment