Bangladesh: Sasa wabakaji kunyongwa hadi kufa |Shamteeblog.

Wahalifu wa ubakaji nchini Bangladesh sasa watanyongwa hadi kufa baada ya Rais wa nchi hiyo, Abdul Hamid kusaini sheria mpya ya hukumu ya kifo kwa wanaopatwa na hatia ya ubakaji.

Mnamo siku ya Jumatatu, baraza la mawaziri la Bangladesh lilipitisha sheria kuongeza hukumu dhidi ya makosa ya ubakaji kutoka maisha gerezani hadi hukumu ya kunyongwa.

Sheria hiyo ilipitishwa wakati visa vya ukatili dhidi ya wanawake vikiwa vimekithiri katika taifa hilo lililoko kusini mwa Asia.



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post