Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian jana kwenye mkutano na waandishi wa habari amesema, China inatilia maanani suala la nchi za Afrika kupunguziwa na kufutiwa madeni, pia inafanya juhudi kutekeleza wito wa Kundi la Nchi 20 (G20) kuhusu suala hilo.
Bw. Zhao amesema, kutoingilia kati mambo ya ndani ya nchi za Afrika, na kutoweka masharti yoyote ya kisiasa, ni kanuni ya China kwenye kushughulikia suala la madeni ya nchi za Afrika.
Pia amesema China inaendelea kuimarisha mawasiliano na nchi za Afrika, na kushughulikia suala la madeni kwa njia ya mazungumzo ya kirafiki.
Vilevile Bw. Zhao amesema, China na Afrika zitatumia fursa ya maadhimisho ya miaka 20 ya kuanzishwa kwa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), na kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja, ili kuwanufaisha watu wao.
By Mpekuzi
Post a Comment