Miaka 21 ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, fahamu haya |Shamteeblog.

Leo Oktoba 14, 2020 ni siku ya kumbukumbu ya miaka 21 tangu kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Mwl. Nyerere alifariki dunia Alhamis ya Oktoba 14, 1999 Saa 4:30 asubuhi katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas, London nchini Uingereza alipokuwa akipatiwa matibabu. #NyerereDay2020.

Mwl. Nyerere alizaliwa Aprili 13, 1922, Butiama, mkoani Mara, pembezoni mwa Ziwa Nyanza, alikuwa Rais wa kwanza wa Tanzania na ndiye mwasisi wa Itikadi ya ‘Ujamaa na Kujitegemea’.

Aliongoza Tanganyika tangu Mei 1, 1961 hadi Januari 22, 1962 kama Waziri Mkuu na kama Rais kuanzia Disemba 9, 1962 hadi Aprili 25, 1964.

Baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, aliongoza Tanzania kuanzia Aprili 24, 1964 hadi Novemba 25, 1985 kama Rais.

Mwl. Nyerere ni kati ya viongozi wachache wa Afrika ambao wameacha madaraka kwa hiari  baada ya kutawala kwa muda mrefu, akiwa bado anapendwa na wananchi walio wengi katika nchi. Alipostaafu urais mwaka 1985 alirudi kijijini kwake Butiama ambako aliendesha shughuli za kilimo.

Nyerere alifanya hotuba mbalimbali katika mikutano ya ndani na nje ya nchi wakati wa uongozi wake na hata baada ya kustaafu. Alisisitiza mambo mengi kuanzia masuala ya uchumi, siasa na dini n.k lakini haya ni mambo matano ambayo alikuwa akiyasisitiza sana.

1. Dini, ni jambo ambalo alisisiza sana katika hotuba zake, hasa kuwaasa viongozi wasitafute uongozi kwa kutumia dini.

2. Ukabila, suala la ukabila ni jambo nyeti ambalo Nyerere aligusia katika hotuba nyingi alizowasilisha.

Nyerere alikemea suala la ukabila kila wakati alipopata nafasi ya kuzungumza na hakutaka kabisa kuwe na maswali kama wewe ni kabila gani? katika hilo alifanikiwa kwa kiasi kikubwa, si kwa kawaida nchini Tanzania kuulizana kuhusu masuala ya ukabila.

3.Ujinga, maradhi na Umaskini, Mwalimu Nyerere alisisitiza juu ya mambo haya makuu matatu, aliyasisitiza katika kipindi cha Tanganyika na baadae Tanzania. itafanikiwa kuyamaliza basi itakua miongoni mwa nchi itakayoendela zaidi duniani. Katika suala la umasikini alilipinga katika sana katika baadhi ya hotuba zake.

4. Uongozi, katika suala la uongozi, maadili ya uongozi ni jambo aliloliweka mbele sana, miongoni mwao ni viongozi ambao wanaweza kukidhi matarajio ya watanzania.

5. Muungano, katika vitu ambavyo alikua akitamani sana kufanya ni kuunganisha nchi za Afrika Mashariki, na kuwa na uongozi wa pamoja, ingawa hakufanikiwa katika hilo, alifanikiwa katika kuunganisha Tanganyika na Zanzibar mwaka 1994.



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post