Shirika la utangazaji la Uingereza BBC limesema, Kasuku watano wamelazimika kuwekwa kizuizini katika bustani moja huko London, Uingereza kutokana na kuwatolea lugha chafu watalii.
Bustani moja ya wanyamapori nchini Uingereza mwezi wa Agosti mwaka huu ilianza kufuga Kasuku tano, ambao walifundishana lugha chafu.
Bustani hiyo ilipofunguliwa, Kasuku hao walianza kuwatolea lugha chafu watalii. Ili kuzuia Kasuku hao kuwafundisha watoto lugha mbaya, bustani hiyo imeamua kuwatenga Kasuku hao na kuwafundisha upya.
By Mpekuzi
Post a Comment