Mwandishi aliyejichoma moto makao makuu ya Polisi |Shamteeblog.

Na Ibrahim Chawe

Mwandishi wa habari na Mhariri wa mtandao wa Koza Press nchini Urusi amefariki baada ya kujichoma kwa moto karibu na ofisi ndogo ya wizara ya mambo ya ndani ya nchi hiyo.

Irina Slavina Kupitia ukurasa wake wa Facebook Mwandishi huyo aliandika kuwa serikali ya Urusi inahusika katika kifo chake Mamlaka zimethibitisha kupatikana kwa mwili wake ukiwa na majeraha. Slavina amesema kuwa siku ya Alhamisi Polisi walimfanyia upekuzi na baadae kushikilia vitu vyake ikiwa ni pamoja na kompyuta zinazosadikika kutumiwa na moja ya kikundi cha harakati za kidemokrasia nchini humo

Baadhi ya picha za video zimemuonyesha muandishi huyo akiwa katikati ya moto karibu na ofisi za makao makuu ya wizara ya mamvo ya Ndani katika Mjini Nizhny Novgorod, video hiyo pia inamuonyesha mwanaume mmoja akiwahi kumuokoa mwandishi huyo kwenye moto huo akijitahidi kuuzima moto kwa kutumia koti lake kujaribu kuzima moto ili kumuokoa kabla mwandishi hyo hajadondoka na kufariki

Kamati ya uchunguzi nchini Urusi imethibitisha kufariki kwa Slavina anayeishi na mume wake na mtoto mmoja wa kike amefariki lakini imegoma kulihusisha tukio hilo na ukaguzi uliofanyika dhidi yake siku ya Alhamisi

Irina Slavina alikuwa Mhariri wa mtandao wa Koza Press . Mtandao uliojipambanua wa sera zake za uchambuzi wa habari bila upendeleo, alikua ni miongoni mwa watu saba ambao walifanyiwa ukaguzi siku ya Alhamisi kutokana na kuhisiwa kushirikiana na vikundi vinavyoipinga serikali ya nchi hiyo

Mwaka uliopita mwandishi huyo alikamatwa na kuadhibiwa kwa kosa la kutoheshimu mamlaka katika moja ya maandiko yake baadhi ya wanahabari wameiambia BBC kuwa alifanyiwa ukatili na kupigwa kinyume na sheria

Katika ujumbe wake wa facebook amesema kuwa watu 12 walikaguliwa na kunyang’anywa vifaa vyao vya mawasiliano akiwemo mumewe pamoja na mwanae.

Kamati ya uchunguzi imesema kuwa Slavina alikaguliwa kutokana na mahusiano aliyonayo na mfanyabiashara na kiongozi mmoja wa kanisa Mikhail Losilevich ambaye anahusika na kuunda vikundi mbalimbali ya upinzani pamoja na kuendsha mafuzo ya uangalizi wa uvhaguzi

Mwandishi huyo alipigwa faini ya 5,000 roubles (£50) kutokana na kuhudhuria kuongamano la Free People Forum mwezi April mwaka jana wakati serikali ilisema kuwa mwandishi huyo alilipoti taarifa za taasisi ambayo haikusajiliwa rasmi. sheria nchini humo zinabinya uhuru wa vyombo vya habari na kuzima ukosoaji uliopo.

 



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post