Balozi Bana Aitembelea Simba sc |Shamtee.blog

Ikiwa nchini Nigeria katika kujiandaa na mchezo wa hatua ya awali dhidi ya Plateau United ya nchini humo,Klabu ya Simba sc imetembelewa na Balozi wa Tanzania nchini humo Dk.Benson Bana katika kambi ya timu jijini Abuja.

Taarifa iliyochapishwa katika ukurasa wa mitandao ya kijamii ya klabu hiyo ilionyesha kwamba Balozi huyo alitembelea kambi hiyo na kukutana na wachezaji na viongozi pamoja na kukabidhiwa jezi ya klabu hiyo.

”Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Dkt. Benson Bana ametembelea kambi yetu hapa jijini Abuja ambapo amepata nafasi ya kuzungumza na viongozi na wachezaji na pia kukabidhiwa zawadi ya jezi mpya ambayo tutaitumia kwenye Ligi”Ilisomeka taarifa hiyo.

The post Balozi Bana Aitembelea Simba sc appeared first on Sports Leo.



By Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post