Na SAM BAHARI-SHINYANGA
JESHI la Polisi mkoani Shinyanga linawashikilia watu wawili kwa tuhuma ya wizi wa vifaa tiba vyenye thamani ya Shilingi Milioni 26, mali ya Hospitali ya Serikali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Debora Magiligimba alisema tukio hilo lilitokea Oktoba mwaka huu saa 12.00 jioni katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Alisema vifaa hivyo vilivyoibwa vina thamani ya Sh milion 26.
Kamanda Magiligimba aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Madaraka Joseph (32) Muuguzi wa Hospitali Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga mkazi wa mtaa wa Mageuzi na Suka Charles (42) mkazi wa mtaa wa Buzuka katika Manispaa ya Shinyanga.
Akifafanua Magiligimba alisema kuwa mtuhumiwa Suka Charles ni Daktari na mmiliki wa Zahanati ya Suka Wazazi iliyopo Wilayani Kahama na Madaraka Joseph ambaye ni mfanyakazi wa Idara ya Chumba cha Upasuaji katika hospitali hiyo.
Alisema Joseph ambaye ni mfanyakazi katika Idara ya Chumba cha Upasuaji ndiye anaye dhaniwa kuziiba mashine hizo na kwenda kuziuza kwa Suka Charles kwa makubaliano ya Sh milioni 4,000,000 ambapo alishatanguliziwa Sh milioni 2,000,000.
Kamanda Magiligimba alisema Vifaa tiba vilivyoibwa ni pamoja na mashine mbili za kuangalia wagonjwa katika chumba cha Upasuaji aina ya EDAN IM8 na DATA SCOP I zenye thamani ya Sh milioni 26 mali ya Hospitali hiyo.
Magiligimba alivitaja Vifaa tiba vingine kuwa ni pamoja na Patient monitor S/N 301237-M16CO9160006-01. Patient monitor S/N PG 63700-B2, BP machine Accessories O5.
Vifaa vingine ni Cable wires Accessories O7, Medical molecularsieve, Oxygen Concentrator 01 serial No 598, na Oxygen Concentrator Intessty S/N 601. 1/IEC/601-1.
Kamanda Magiligimba alisema kuwa watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazo wakabili mara baada ya upelelezi kukamilika.
from Author
Post a Comment