‘Focus’ ya Coolpixie yatua mtaani |Shamteeblog.

NA CHRISTOPHER MSEKENA

LEBO inayokuja kwa kasi barani Afrika kutoka Afrika Kusini, Madambad Entertainment, amewashukuru mashabiki zake kwa mapokezi makubwa ya wimbo, Focus wa msanii wao, Coolpixie.

Akizungumza na MTANZANIA, bosi wa lebo hiyo, Madam Bad alisema ndani ya muda mfupi tangu walipoachia wimbo huo kwenye mitandao ya kuuza na kusikiliza muziki, mwitikio umekuwa mkubwa tofauti na walivyodhani.

“Tumeachia audio ya Focus katika mitandao yote ya muziki kama vile Tidal, YouTube, Apple Music, Spotify, Amazon Music, Deezer na mingine kwahiyo mashabiki zetu wapya wanaweza kuupata na sio muda mrefu utaanza kusikika kwenye redio hapo Bongo kikubwa tunaomba sapoti,” alisema Madam Bad.



from Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post