NA DAMIAN MASYENENE, MWANZA
MSANII anayefanya vizuri mkoani Mwanza, Jackson John a.k.a J Boy Tiger, ametamba kuwa yeye ndio msanii anayelibeba Jiji hilo kwa sasa kwenye tasnia ya muziki.
Akizungumza na MTANZANIA , J Boy ambaye ni msomi wa Chuo Kikuu alisema anawashukuru wasanii wakubwa wa Mwanza kama H Baba na Coyo Mc wamekuwa wakimpa sapoti mpaka sasa ana heshima kubwa ndani na nje ya Jiji hilo.
“Nilianza rasmi muziki mwaka 2017 na mipango yangu kimuziki ni mikubwa sana ikiwamo nikufika mbali kisanaa ndani na nje ya nchi yangu ili niweze kulitangaza Taifa langu Tanzania kama ambavyo naitangaza Mwanza kwa sasa, kabla ya mwaka kuisha pia nitaachia ngoma yangu mpya,” alisema J Boy.
from Author
Post a Comment