King 98 aibuka upya na ‘I Bet’ |Shamteeblog.

NA CHRISTOPHER MSEKENA

STAA wa muziki nchini Zimbabwe, Ngoniszone Dondo a.k.a King 98, ameachia wimbo mpya, I Bet ukiwa ni mwendelezo wa kuwapa raha mashabiki baada ya kufanya vizuri na wimbo, Kachiri aliomshirikisha Diamond Platnumz.

King 98 anayesimamiwa na Impala Music Group, ameliambia MTANZANIA jana kuwa ndani ya ndani ya I Bet, ameonyesha utundu mkubwa wa kuandika, kuimba Afro Pop na kurap hivyo anatamani kila mmoja asikilze na kutazama video ya ngoma hiyo.

“Ndani ya I Bet nimezungumzia simulizi ya jamaa ambaye anampenda kimapenzi mrembo lakini msichana huyo amekuwa akimuumiza na kumkatisha tamaa. Wimbo huu mpya tayari upo kwenye mitandao yote na chaneli yangu ya YouTube,” alisema King 98.

Aliongeza kwa kumshukuru prodyuza Cog Beats na s2kizzy kwa kutengeneza ngoma hiyo ambayo tayari imeanza kufanya vizuri ndani na nje ya Zimbawe.



from Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post