Kwisha Habari Yao |Shamtee.blog

Licha ya kufanya fitina nyingi nje ya uwanja hatimae klabu ya Plateau United wamekubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Simba sc ya Tanzania katika mchezo wa hatua ya awali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika.

Bao pekee la Simba sc liliwekwa kimiani na Cletous Chama dakika ya 54 ya mchezo ambapo licha ya Wanigeria hao kutumia nguvu nyingi hawakufanikiwa kupata bao mpaka dakika 90 za mchezo zilipokamilika.

Ushindi huo umeifanya Simba sc kuvunja mwiko wa miaka 41 ya kutozifunga nyumbani kwao timu za Nigeria huku mechi ya marudiano ikitarajiwa kufanyika wiki ijayo jijini Dar es salaam.

“Ulikuwa mchezo mgumu, wana nguvu na walijaribu kiufundi kutafuta goli lakini nawapongeza wachezaji wangu sababu dakika zote 90 walikuwa wanakimbia kuzuia. Nafikiri tunatakiwa kuwa na furaha sana na ushindi. Matokeo mazuri lakini bado hatujamaliza sababu wiki ijayo tuna dakika 90 zingine.”- Alisema Kocha Sven Vandebroek

The post Kwisha Habari Yao appeared first on Sports Leo.



By Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post