Makoi achaguliwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Moshi DC |Shamteeblog.

Na MWANDISHI WETU

Diwani wa Kata ya Okaoni, Morris Makoi(CCM) amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Moshi DC Mkoani Kilimanjaro baada ya kuibuka na ushindi wa kura 30.

Uchaguzi huo uliyofanyika juzi mkoani Kilimanjaro ambapo Makoi aliibuka kuwa mshindi kwa kura 30 huku mpinzani wake, Dickson Tarimo ambaye ni Diwani wa Kata ya Makuyuni Jimbo la Vunjo akiambulia kura 16.

Diwani wa Kata ya Makuyuni jimbo la Vunjo aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Moshi, Dickson Tarimo akisaini matokeo ya kukiri ameshinda

Halmashauri hiyo ina wajumbe wa baraza la madiwani 48, ambapo madiwani ni 43 na wabunge watano, katika madiwani hao wa kata ni 32 na waviti maalumu 11.

Hata hivyo wajumbe wawili hawakupiga kura mbunge mmoja wa viti maalumu, Shaly Raymond hakuhudhuria na diwani wa kata ya Kibosho Kati hakupiga kura.

Kwa upande wake, Makoi ambae ndio ameshinda nafasi hiyo alisema kuwa uchaguzi huo umefanyika kwa uwazi huku akiipongeza kamati ya siasa ya Wilaya.

“Uchaguzi umekwenda vizuri kabisa niwapongeze kamati ya siasa ya wilaya yetu kwa kusimamia mchakato vizuri sana, nataka niwaombe wabunge twende tukachape kazi tukamilishe ahadi za Rais wetu Dk. John Magufuli ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa Halmashauri mpya ya wilaya ya Vunjo,”alisema Makoi.



from Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post