WASHINGTON, MAREKANI
MSHIRIKA wa karibu wa Rais Donald Trump, ambaye pia aliwahi kuwa Gavana wa Jimbo la New Jersey, Chris Christie, amemtaka Trump kukubali matokeo ya uchaguzi uliompa ushindi mpinzani wake wa karibu, Joe Biden.
Katika matamshi yake, Chris Christie, amekitaja kikosi kinachomshauri Trump kwa masuala ya kisheria kama aibu na fedheha kwa taifa.
Donald Trump amekataa kubali kushindwa, kwa madai kuwa uchaguzi huo ulikumbwa na dosari, madai ambayo hadi sasa ameshindwa kuyathibitisha.Baadhi ya wajumbe wa chama cha Republican, wameonekana kuunga mkono madai ya Trump, huku baadhi yao wakionekana kuwa na msimamo tafauti na ule wa chama chao.
Muhula ulioainishwa kwa ajili ya kuthibitishwa kutangazwa matokeo ya uchaguzi nchini Marekani ni jambo la lazima; na muhula huo unamalizika tarehe 14 mwezi Disemba mwaka huu, na baada ya hapo baraza la Electoral College litaundwa ili kupiga kura.
Itakumbwa kuwa, timu ya kampeni ya uchaguzi ya Trump hadi sasa imepinga na kukataa kukubali matokeo ya uchaguzi wa rais nchini Marekani na imewasilisha mashtaka katika majimbo kadhaa dhidi ya kile ilichokitaja kuwa kujiri udanganyifu na uchakachuaji wa kura katika uchaguzi wa rais wa Marekani.
Hata hivyo mashtaka hayo yamepingwa katika majimbo kadhaa ya Marekani.
Siku ya Jumamosi, Trump alipata pigo katika azma yake ya kupinga matokeo ya jimbo la Pennsylvania, baaada ya jaji kutupilia mbali kesi ya madai ya wizi wa kura baada ya kuhesabiwa upya.
AP
from Author
Post a Comment