WARSAW, POLAND
SHIRIKA moja la kimataifa la kuwaunga mkono watoto limetangaza kuwa, kuanzia mwaka 2005 hadi sasa watoto wapatao watano wamekuwa wakiuawa au kujeruhiwa kila siku nchini Afghanistan na kuifanya nchi hiyo kuwa hatari zaidi dunia kwa watoto.
Shirika la Kimataifa la Kutetea Haki za Watoto la Save the Children limetangaza kuwa, Afghanistan ni nchi hatari zaidi kwa toto duniani na kubainisha kwamba, zaidi ya watoto 26,000 wameuawa au kujeruhiwa nchini humo tangu mwaka 2005.
Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Save The Children kuanzia mwaka 2005 hadi sasa na kwa makadirio ya kati kila siku watoto watano wamekuwa wakiuawa au kujeruhiwa nchini Afghanistan.
Shirika hilo aidha limeitaka serikali ya Uingereza kutumia nafasi na ushawishi wake katika uga wa kimataifa kutoa taarifa ya kuzuia kutumiwa silaha za milipuko katika maeneo yenye watu wengi duniani.
Watoto wa Yemen ni miongoni mwa watoto wanaotaabika pia duniani kutokana na hujuma na mashambulio ya kijeshi ya SaudiArabia
Sehemu nyingine ya ripoti hiyo ya Shirika la Save the Children inasema kuwa, kuanzia mwaka 2017 hadi 2019 shule nchini Afghanistan zilishambuliwa mara 300 ambapo kufuatia hujuma na mashambulio hayo wanafunzi na walimu wapatao 410 waliuawa au kujeruhiwa.
Kadhalika ripoti hiyo inaeleza kwamba, watoto milioni 7 nchini Afghanistan wanakabiliwa na baa la njaa huku wengine milioni 3 walio na umri wa chini ya miaka mitano wakikabiliwa na lishe duni.
AP
from Author
Post a Comment