Na Mwandishi wetu, Globu ya Jamii
JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanikiwa kumkamata AMANI MWANDENGA [30] Mkazi wa Ihango na kisha kumfikisha mahakamani kwa tuhuma ya kosa la kubaka mtoto wa miaka 09.
Katika taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya SACP, Ulricho Mtei imesema kuwa mnamo tarehe 19/05/2020 majira ya saa 12:00 mchana huko Kijiji cha Ipinda, Kata ya Ihango, Wilaya ya Mbeya vijijini, mtuhumiwa alimkamata kwa nguvu kisha kumbaka mtoto wa miaka 09 na kumsababisha maumivu makali.
Mtuhumiwa alikamatwa na mnamo tarehe 11/06/2020 alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi – Mkoa wa Mbeya CC NO.156/2020 kwa kosa la kubaka. Ushahidi wa shauri hili ulitolewa na jumla ya mashahidi watano na mnamo tarehe 28/12/2020 Mahakama ilimkuta na hatia ya kwenda jela kifungo cha maisha.
Hata hivyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia wakazi wawili wa Mtakuja katika Mji Mdogo, Mbalizi 1. Vesto Timoth [18] na 2. Michael Mwile [18] wakiwa na mali za wizi.
Tarifa hiyo imaeleza kuwa Watuhumiwa walikamatwa mnamo tarehe 28.12.2020 majira ya saa 09:45 asubuhi katika msako uliofanyika katika Mji Mdogo wa Mbalizi na kukamatwa wakiwa na TV moja nchi 14 aina ya Sundar flat screen mali ya wizi. Upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani.
By Mpekuzi
Post a Comment