Safina Sarwatt, Kilimanjaro
Mashindano ya mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathoni 2021 yamezinduliwa rasmi mkoani Kilimanjaro ambapo jumla ya mataifa 55 wanatarajiwa kushiriki.
Akizungumza katika uzinduzi huo huo uliofanyika juzi Mkuu wa wilaya Moshi, Alhaji Kundya, amesema kuwa washiriki wote watapimwa corona kabla ya kushiriki na kwamba wangeni wanaoingia nchini watatakiwa kuwa vyeti vinavyothibithishwa hawana maabukizi ya virusi vya corona.
Kundya amesema mbio hizo zinasaidia katika kukuza utalii na biashara mkoani humo na Tanzania kwa ujumla na kwamba yupo tayari kushirikiana na waandaji katika kushughulikia changamoto mbalimbali zilizopo ili mbio ziweze kuandikisha idadi kubwa.
Amesema mbio hizo zinasajili takriban washiriki 12,000 na waandaaji wanashindwa kuongeza idadi hiyo kutokana na changamoto na barabara kuwa nyembamba.
“Tulishaanza kuzungumza namna gani tunaweza kutanua barabara zetu ili mbio hizi ziweze usajili washiriki wengi zaidi kwani kwa sasa ikifikiwa idadi maalumu waandaji wanalazimika kufunga usajili ili kuhakikisha wanaendana na matakwa na miongozo ya Shirikisho la Riadha la Kimataifa, (IAAF) pia kujiridhisha kuwa wanaweza kutoa huduma kama Maji na hHduma ya Kwanza ,”amesema.
Kwa upande wake Meneja wa bia ya Kilimanjaro, Irene Mutiganzi ambaye pia Meneja wa kinywaji cha Grand Malt, amesema wanajivunia kuwa Wanadhamini wakuu wa mbio hizo kwa mwaka wa 19 sasa tangu kuanza kwa mbio hizo nakwamba ni jambo la kizalendo na kuangaza Tanzania.
Amesema wamejiandaa vema kwa ajili ya mbio Kilimanjaro Marathon huku wakitenga Sh milioni 25 kwa ajili ya zawadi za washindi wa kwanza upande wanaume na wanawake ambapo washindi watajinyakulia Sh milioni 4 kila mmoja na Watanzania upande wanaume na wanawake watapata million 1.5 kama motisha.
Naye Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo, amesema kampuni hiyo imedhamini mbio za Kilometa 21 na kwamba mbio za mwaka huu nizatofauti na miaka iliyopita kutokana na mwamko mkubwa wa washiriki.
Wadhamini wengine ni pamoja Kilimanjaro Drinking Water, TPC Limited, Unilever Tanzania, Simba Cement, Absa Bank Tanzania na watoa huduma rasmi keys Hotel, waandaji Kilimanjaro Marathon Company na Executive Solution ambao ni waratibu.
Mkurugenzi wa Executive Solution, Aggrey Marealle amesema tayari zaidi ya washiriki 3,917 katika mbio za kilometa 42, kilometa 21 na tano wamejisajili.
from Author
Post a Comment