Kamati ya Uongozi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA) inaanza ziara ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa shughuli za urasimishaji wa ardhi na biashara katika mikoa ya nyanda za juu kusini.
Akieleza kuhusu ziara hiyo Jijini Dodoma katika mahojiano maalum yaliyofanyika Januari 23, 2021, Mratibu wa Mpango huo, CPA, Dkt. Seraphia Mgembe amesema kuwa kamati hiyo itashiriki katika kazi mbalimbali ikiwemo zoezi la utoaji hati za hakimiliki za kimila za kumiliki ardhi katika halamshauri ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa na uwekaji wa jiwe la msingi la jengo la Ofisi ya masjala ya ardhi katika Kijiji cha Kapya wilayani Mbarali mkoani Mbeya.
Akieleza zaidi kuhusu ziara hiyo Dkt. Mgembe amesema kuwa ziara hiyo ya wiki moja inaanza leo Januari 24, 2021 hadi Januari 31,2021.
MKURABITA imekuwa ikiwezesha wanachi kipitia urasimishaji ardhi na biashara katika halmashuri mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kuwawezesha kiuchumi kama ilivyo dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano.
By Mpekuzi
Post a Comment