Na Brighiter Masaki, Dar es Salaam
Nguli wa Rhumba, Koffi Olomide kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, amewasili nchini Tanzania usiku wa kuamkia leo kwa ajiri ya kufanya show yake ya Mahaba ya Rhumba itakayofanyika usiku wa leo Februari 13, katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, Koffi amesema kuwa Watanzania wajiandae kwa burudani nzuri.
Aidha, Koffi ametumia mwanya huo kuwakumbusha Watanznai kwambayuko Dar es Salaam baada ya kutumbuiza kionjo cha wimbo mpya wa Leo leo aliofanya na Mwanadada Nandy ikiwa ni kiashiria cha burudani kali atakayoitoa leo kwa Wana-Dar es Salaam ukiwa ni uski wa kuamkia siku ya Wapendanao, Februari 14.
“Nina wimbo maalum kwa Watanzania watarajie burudani ya kutosha bila kusahau suprizi kutokea kwa timu yangu nzima ya Mopao, hivyo wasipange kukosa Mahaba ya Rhumba,” amesema Koffi.
Katika onyesho hilo, Koffi atasindikizwa na msanii kutokea Tanzania Faustina Mfinanga, ‘Nandy’ ambaye kwa sasa wanatamba na wimbo wao wa Leo leo ambao watautumbuiza kwa mara ya kwanza .
from Author
Post a Comment