NA YEREMIAS NGERANGERA…NAMTUMBO
Naibu waziri ofisi ya Raisi TAMISEMI David Silinde ameridhishwa na ujenzi wa bweni katika shule ya sekondari Selous na ujenzi wa bwalo katika shule ya sekondari Nasuli baada ya kufanya ziara ya kukagua ujenzi huo na kuridhishwa na hatua za ujenzi wa majengo hayo na kiasi cha fedha kilichotumika .
“Nampongeza mkuu wa wilaya Namtumbo kwa usimamizi thabiti,nawapongeza wakuu wa shule kwa kuwa fedha hizo za ujenzi zinafika moja kwa moja katika shule na kusimamia utaratibu wa ujenzi hatua kwa hatua ,nawapongeza wataalamu wa Halmashauri wakiongozwa na mkurugenzi wa Halmashauri pamoja na mkuu wa idara ya elimu sekondari kwa kufuatilia hatua kwa hatua ujenzi huo” alisema naibu waziri huyo.
Mkuu wa shule ya sekondari Selous bwana Bernard Nyoni pamoja na kuishukuru serikali ya Raisi John Pombe Magufuli kwa kutoa fedha milioni 80 ili kujenga bweni kuwasaidia wanafunzi waliokuwa wanatembea umbali mrefu kufika shuleni na mara kadhaa wanafunzi hao walikuwa wanakumbana na hatari kubwa ya kuvamiwa na wanyama tembo nyakati za asubuhi na jioni.
Nyoni alisema kitendo cha serikali kuliona tatizo hilo ni ukombozi mkubwa kwa wanafunzi wanaosoma katika shule ya sekondari hiyo kwa sasa tofauti na huko nyuma ambapo walishuhudia wazazi wengi wakihamisha watoto wao kwenda katika shule zingine lakini kwa sasa wazazi wengi nao wanaomba kuwaleta watoto wao hapa ni matokeo ya ujenzi huu wa bweni alisema Nyoni.
Naye mkuu wa shule ya sekondari Nasuli bwana Raphael Komba alisema shule ilipokea kiasi cha shilingi milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa bwalo na kadiri ya makadirio ya gharama ya ujenzi wa bwalo hilo fedha hizo hazitoshi kukamilisha ujenzi mpaka hatua za mwisho za kuanza matumizi.
Mhandisi wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Hassan Kinonono alidai makadirio ya gharama za ujenzi wa bwalo hilo ni milioni 150 lakini halmashuri kupitia vikao vyake ilijitahidi kuangalia uwezekanao wa kupata fedha kutoka katika miradi mengine iliyobakiza fedha ili kuhakikisha jengo hilo linakamilika.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo bwana Evance Nachimbinya alimhakikishia naibu waziri huyo kuwa Halmashauri itahakikisha jengo hilo linaisha kwa muda uliopangwa na ofisi yake itasimamia upatikana wa fedha za kumalizia jengo hilo .
By Mpekuzi
Post a Comment