RWEIKIZA ACHANGIA MILIONI 8 KLINIKI YA KIBIRIZI. |Shamteeblog.


Na Abdullatif Yunus Michuzi TV.

Dkt Jasson Samson Rweikiza anaendelea na Ziara yake mchana huu katika Jimbo la Bukoba Vijijini kwa kutembelea Kata mbalimbali za Jimbo lake ambapo amefika Kata KIBIRIZI na kutoa Shukrani zake.

Mhe. Rweikiza amefika Kata KIBIRIZI na kutembelea Kliniki ya Mama na Mtoto ya Rwakaigwa inayojengwa katika Kijiji Ombueya na kujionea jitihada Zilizofanyika kupitia mchango wake wa Awali alioutoa hapo mwanzoni.

Baada ya kuwasili eneo hilo Mhe. Rweikiza amefurahishwa na jinsi mchango wake wa Shilingi Laki Nne ulivyosaidia na hivyo kutoa Milioni 8 ambazo zitasaidia kuendeleza Ujenzi wa jengo hilo na kulifanya liwe la Kisasa.

Mchango huo unakuja siku chache zikiwa zimesalia kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani Machi 08, 2021ambapo wanawake Kijiji hicho wamekuwa wakitembea umbali wa Km 6 kufuata Kliniki kwenye Zahanati ya Kijiji, na hivyo kwa nyakati tofauti wakashukuru ujio wa Mbunge kufika  kijijini hapo.

Sambamba na hilo Mhe. Rweikiza amekamilisha ahadi yake ya Kulipa mshahara wa walinzi wawili jumla ya Shilingi laki Tano na kabla ya kuondoka Kata hiyo amefika Shule ya Sekondari Kibirizi na huko kuwashukuru na kuwaachia laki Mbili ya Sukari na Mipira miwili.



 

Mhe. Rweikiza akikabidhi Shilingi Laki Mbili na Nusu Kama ahadi yake aliyoitoa ya kulipa Mshahara wa Mlinzi wa Kliniki Rwakaigwa, na kukabidhi laki Mbili na Nusu nyingine kwa Mlinzi wa Zahanati ya Kijiji.
 Pichani Mhe. Rweikiza akikabidhi Mipira miwili kwa Kiranja wa Michezo Shule ya Sekondari Kibirizi.
Mkazi wa Kijiji Kibirizi ambaye hakufamika Mara moja akionekana kutabasamu baada ya Mbunge Rweikiza kutoa Milioni 8 za Ujenzi wa Kliniki yao ya Rwakaigwa.


By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post