RWEIKIZA AKAMILISHA AHADI YA MILIONI 21 JIMBONI KWAKE. |Shamteeblog.



Na Abdullatif Yunus MichuziTv.

Dkt Jasson Samson Rweikiza Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini, ameanza Ziara  yake ya Kushukuru na kukamilisha ahadi alizozitoa kipindi cha Kampeini, huku akibaini Miradi mipya na changamoto mpya  katika Jimbo la Bukoba Vijijini kwa kutembelea Kata mbalimbali za Jimbo lake ambapo ameanza na  Kata za Butelankuzi, Kibirizi na Kagya ziara iliyoanza Februari 24,2021.

Mhe. Rweikiza amefika Kata Butelankuzi na kukutana na Walimu na Wanafunzi wa Shule za Sekondari  Tunamkumbuka, pamoja na Shule ya Sekondari  Kibirizi na ya Kata Kibirizi ambapo katika Shule ameshukuru kwa namna walivyompigia Kura kwa Wingi na Kuwaachia Pesa Shilingi laki Mbili kila Shule za Sukari ya Uji pamoja na Mipira miwili miwili ya Michezo

Aidha kwa Upande Mwingine Mhe. Rweikiza akiwa Kata Kibirizi ametembelea Kliniki ya Mama na Mtoto ya Rwakaigwa inayojengwa katika Kijiji Ombueya na kujionea jitihada zilizofanyika kupitia mchango wake wa Awali alioutoa hapo mwanzoni.

Baada ya kuwasili eneo hilo Mhe. Rweikiza amefurahishwa na jinsi mchango wake wa Shilingi Laki Nne ulivyosaidia na hivyo kutoa Milioni 8 ambazo zitasaidia kuendeleza Ujenzi wa jengo hilo na kulifanya liwe la Kisasa.

Mchango huo unakuja siku chache zikiwa zimesalia kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani Machi 08, 2021ambapo wanawake Kijiji hicho wamekuwa wakitembea umbali wa Km 6 kufuata Kliniki kwenye Zahanati ya Kijiji, na hivyo kwa nyakati tofauti wakashukuru ujio wa Mbunge kufika  kijijini hapo.

Mhe. Rweikiza amekamilisha Ziara yake ya Siku ya kwanza Tangu kuchaguliwa kwa Kufika Kata Kagya ambapo pamoja na Mambo mengine ametoa Shilingi Milioni 12 kwa ajili ya Ujenzi wa Daraja la Omkibimbili ambalo limekuwa Kero kipindi cha Mvua, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aloitoa wakatti wa kuomba ridhaa Mwaka Jana.

Sambamba na hilo Mhe. Rweikiza amekamilisha ahadi yake ya Kulipa mshahara wa walinzi wawili jumla ya Shilingi laki Tano na kabla ya kuondoka Kata hiyo amefika Shule ya Sekondari Kibirizi na huko kuwashukuru na kuwaachia laki Mbili ya Sukari na Mipira miwili.

Mbunge Rweikiza akishuhudia Ujenzi wa kalavati limaloumganisha Kijiji cha Kibirizi na Ombueya ambapo sehemu imekuwa Kero kipindi cha Mvua.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kibirizi Wakifurahia na Mbunge wao Mara baada ya kuwapa Shilingi laki Mbili na Mipira miwili
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Tunamkumbuka Wakifurahia na Mbunge wao Mara baada ya kuwapa Shilingi laki Mbili na Mipira miwili




By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post