Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
KLABU ya Simba ya Tanzania imeendelea kuweka rekodi mpya na nzuri katika soka la Tanzania baada ya kuendelea kupata ushindi ugenini katika michezo yake ya Kimataifa.
Simba SC imepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AS Vita Club katika dimba la Stade de martyrs mjini Kinshasa nchini DR Congo. Simba SC iliweka rekodi hiyo ya ushindi ugenini mara ya mwisho dhidi ya Plateau United ya Nigeria kwa bao 1-0.
Katika mchezo wa kwanza wa Kundi A bao pekee la Simba SC limefungwa kwa mkwaju wa Penalti na Mshambuliaji Chris Kopa Mushimba Mugalu limeipa ushindi Wekundu wa Msimbazi na kuifanya kuwa timu ya kwanza kupata ushindi katika ardhi ya DR Congo dhidi ya AS Vita.
Mchezo huo uliokuwa wa kasi dakika zote 90, Simba SC walianza kucheza kwa nidhamu ya hali ya juu kulita heshima ya Vita Club wakiwa nyumbani. Mara ya mwisho timu hiyo zilikutana msimu wa 2018-2019 na Simba SC walikubali kichapo cha bao 5-0 katika uwanja huo huo.
Hata hivyo baada ya ushindi huo Simba watacheza mchezo wa pili dhidi ya Al Ahly SC ya Misri, Februari 23, 2021 katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa sasa Simba inaongoza Kundi ikiwa na alama 3 wakiwa Kundi moja na timu za Al Ahly SC, Al Marreikh ya Sudan na AS Vita Club.
By Mpekuzi
Post a Comment