Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Washindi 448 wa kampeni ya NMB MastaBata Sio Kikawaida wamekamilisha miezi mitatu ya droo hiyo wiki hii baada ya kujinyakulia zawadi mbalimbali za vifaa vya nyumbani, fedha taslimu, simu za mkononi na safari za kitalii ambapo thamani ya zawadi zote ni Shilingi Milioni 200.
Droo hiyo imehitimishwa katika fainali iliyofanyika Machi 4, 2021 makao makuu ya Benki ya NMB jijini Dar es Salaam kwa kupatikana washindi 12 ambao wawili kati yao walichagua zawadi ya safari ya kitalii itakayojumuisha watu wawili kwa siku nne, safari hizo ni Serengeti, Ngorongoro na Visiwa vya Zanzibar.
Waliobaki walichagua vifaa vya nyumbani ambavyo vilikuwa ni Runinga kubwa (Smart TV) yenye king’amuzi cha Dstv kilicholipiwa kwa miezi mitatu, Jokofu la milango miwili, simu ya mkononi aina ya Samsung Galaxy Note 20, Microwave, Mashine ya kuchuja maji (Water Dispenser) na computer mpakato (Laptop) iliyounganishwa na Printer.
Aidha, washindi hao ni Mohamed Said Ali aliyechagua vifaa vya nyumbani, Miriam Aidan Mongii (vifaa), Ally Abubakary Ally (vifaa), Indra Pratap Narain Pathak alichagua safari ya kitalii pamoja na Abshir Farah Gure pia alichagua safari.
Washindi waliobakia wote walichagua vifaa vya nyumbani ambao ni Mango Mechris Christopher, Mohamed Hisham Mohamed Nouman, Job Lay Naman, Clara Cynthia Mwinchumu, Alice W. Mariki, Harid Valentino Gange na Christabel Ilona Hiza.
Akizungumza katika hafla ya fainali hiyo jijini Dar es Salaam wiki hii, Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha, Benedicto Baragomwa alisema kwenye shindano hilo katika fainali iliyohusisha washindi 12, kila zawadi ilikuwa na thamani ya Sh Mil 8 hivyo jumla ya Sh Mil 96 zilichukuliwa katika fainali.
“Ukiangalia zawadi za mwisho zinahusisha vifaa vya nyumbani na mbuga za wanyama ikiwemo Serengeti na Ngorongoro pamoja na Visiwa vya Zanzibar, maana yake tunataka kuimarisha utalii wa ndani. Vilevile msingi wa shindano hili ni kutaka wateja wetu wapunguze matumizi ya fedha taslimu, ndiyo maana tulitaka kila anayetumia kadi kufanya miamala kuwa sehemu ya washindi,” alisema Baragomwa.
Kwa upande wake mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Nchini (GBT), Elibariki Sengasenga alisema anawapongeza NMB kwa ubunifu wao lakini pia kwa kipindi chote cha miezi mitatu walipokuwa wakiendesha kampeni hiyo walifuata taratibu zote za bodi hiyo.
“Washindi wote waliopatikana kwa kipi di cha kiezi mitatu ya kampeni hii walipatikana kwa njia za halali, hakukuwa na kona kona wala ujanja. Waliopata fedha taslimu walipewa na walioshinda vifaa vya nyumbani walikabidhiwa, pongezi za kipekee nazipeleka kwa uongozi wa NMB kwa ubunifu mkubwa na wa kipekee kwa kuwa karibu na wateja wao,” alisema Sengasenga.
from Author
Post a Comment