Na Woinde Shizza, Michuzi Tv-ARUSHA
Mkuu wa wilaya ya Arumeru mkoani Arusha,Jerry Muro ametamka ya kwamba msimamo wa Rais wa Tanzania,Dkt John Magufuli kuhusu kutoruhusu uingizaji wa chanjo za corona hapa nchini ni wa kishujaa kwa kuwa watanzania hawawezi kutumika kama majaribio.
Pia amewashauri baadhi ya viongozi wa dini nchini kutoyumba kiimani kwa kuwa baadhi yao wamegawanyika na kukosa msimamo kutokana na ugonjwa wa corona.
Muro,alitoa kauli hiyo juzi katika kanisa la kiinjili na Kilutheri nchini (KKKT) usharika wa Enaboishu wakati wa ibada ya shukrani ya familia ya Elphace Mollel iliyopo mtaa wa Oloigero.
Akizungumza kanisani hapo Muro alisema kwamba Rais Magufuli hajapinga ujio wa chanjo ya corona lakini alichopinga ni chanjo hizo kutumika kwa watanzania kama majaribio.
Muro,alisema kwamba Rais Magufuli atawavusha watanzania salama katika janga la Corona na anathamini watu wake na hivyo msimamo wake wa kuzipinga chanjo hizo za majaribio unapaswa kuungwa mkono.
“Msimamo wa Rais Magufuli kutotaka chanjo za corona kutumika kama majaribio kwa watanzania ni wa kishujaa sio kwamba amekataa chanjo zisiletwe nchini lazima tuelewane huyu Rais wetu anawathamini watu wake sana “alisema Muro
Hatahivyo,aliwashauri baadhi ya viongozi wa dini kuwa na msimamo katika imani kwa kuwa wao wamepewa jukumu la kuwachunga kondoo na sio kuwatia hofu.
Awali Mchungaji aliyeongoza ibada hiyo,Samwel Laiser alisema kwamba pamoja na serikali kupitia wizara ya afya kutoa mwongozo katika kupambana na ugonjwa wa Corona lakini watanzania wanapaswa kumtegemea Mungu kwanza.
Alisema kwamba watanzania wanapaswa kuondokana na hofu katika kipindi hiki kwa kuwa ugonjwa wa corona ni janga litakalopita na kuwasihi wasimame imara muda huu kumtegemea Mungu katika maombi,sala na shukrani.
“Neno na Mungu ndilo linalotia nguvu endeleeni kumtumikia Mungu sote tuondoe hofu na mashaka pamoja na wizara ya afya kutoa maelekezo lakini maombi yawe nambari moja “alisema Laiser
Akitoa shukrani katika ibada hiyo kwa niaba ya familia Dr.Ezekiel Mollel alisema kwamba anamshukuru Mungu kumponya mama yake mzazi aliyelazwa mahututi katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) akipumulia mashine na ameamua kutoa shukrani kumshukuru Mungu.
Mollel,alisema watanzania wanapaswa kumshukuru Mungu katika janga la corona na kumuombea Rais Magufuli kwa kuwaondolea hofu kwa kuwa awali hofu ilikuwa inawaua kuliko corona.
Mchungaji aliyeongoza ibada hiyo ya Shukrani Samweli Laizer akiongea na waumini ambapo alisema watanzania wanapaswa kumuamini Mungu.
Dkt.Ezekiel Mollel akitoa neno la Shukrani kwa niaba ya familia Katika kanisa la KKKT usharika wa Enaboishu mtaa wa Oloigero ambapo alisema ni vyema watanzania tukamlilia mungu maana haku linaloshindikana kwake yeye.
viongozi mbalimbali waliomsindikiza Dkt Ezekiel Mollel kutoa sadaka ya Shukrani wakifatilia ibada hiyo
waumini wakiwa Katika ibadaBy Mpekuzi
Post a Comment