DIWO YATOA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WANAWAKE WAJASIRIAMALI WILAYANI MUHEZA |Shamteeblog.

 

Amiri Msuya kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Halamshauri ya Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga aizungumza wakati akifunga mafunzo hayo kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Dira Women Organization (DIWO) Shamsa Danga kushoto ni Afisa Maendeleo ya Jamii wilayani Muheza Damiano Apolinary

 

Mkurugenzi wa Taasisi ya Dira Women Organization (DIWO) Shamsa Danga akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafunzo hayo
Afisa Maendeleo ya Jamii wilayani Muheza Damiano Apolinary  akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo
Meza Kuu wakifuatilia matukio mbalimbali
AFISA uendeshaji Biashara kutoka SIDO Tanga GladnessFoya akizungumza wakati wa mafunzo hayo
 Mwezeshaji wa Mafunzo ya Sabuni na Vipodozi Farida Swalehe akitoa elimu
Mkurugenzi wa Taasisi ya Dira Women Organization (DIWO) Shamsa Danga akipanga bidhaa mbalimbali wakati wa mafunzo hayo
Sehemu ya wakina mama wajasiriamali walioshiriki mafunzo hayo

TAASISI ya Dira Women Organization (DIWO) imetoa mafunzo ya  kuwajengea uwezo wanawake wajasiriamali wa Kikundi cha TADAHA Women Products kilichopo Kibanda kwa Semkopi wilayani Muheza Mkoani Tanga ili waweze kutengeneza bidhaa zenye ubora na viwango vinavyokubalika.

Mafunzo hayo yamedhaminiwa na Taasisi ya Diwo ambao wamekwenda kuwajengea uwezo wanawake hao wajasiriamali ili watumie ujuzi huo kujikomboa kiuchumi ikiwemo kutengeneza bidhaa ambazo zitakuwa na ubora mzuri.

Akizungumza wakati wa Mafunzo hayo,Mkurugenzi wa Taasisi ya Dira Women Organization (DIWO) Shamsa Danga yaliyofanyika wilayani Muheza ambapo alisema mafunzo hayo yatawawezesha wanawake hao wajasiriamali kujengewa uwezo wa kusimama imara na kutumia  fursa zilizopo ili kujipatia kipato.

Alisema kwamba awali waliwakuta wanatengeneza sabuni bila ya kupata mafunzo yalio rasmi huku wakikabiliwa na vikwazo mbalimbali na ndipo walipoona wawapatie mafunzi ambayo yatawawezesha kufanya shughuli za ujasiriamali wao kwa tija kubwa na mafanikio kuliko ilivyokuwa awali.

“Kikundi hiki tulipokutana nacho tuliwakutana na cheti lakini hakikuwa kinajulikana kisheria na nilitamani wajisajili ili waweze kujulikana.Cha kwanza niliwasaidia kusajili jina la kikundi chao cha TADAHA Women Products Brela na kusaidia alama za bidhaa za kibiashara (Barcode) ”Alisema

Alisema kwa sababu kama unatengeneza bidhaa zao bila kuwa na alama za
kibiashara huwezi kutanua soko lako sababu kuna sehemu nyingine huwezi kuuza kama super market na maduka makubwa lakini hauwezi. Lakini pia wanatakiwa wapate alama ya ubora wa bidhaa  kutoka TBS.

Akizungumzia vikwazo ambavyo wanakumbana navyo wanawake wajasiriamali alisema moja wapo ni kutokupewa nafasi hivyo viongozi wa maeneo mbalimbali hapa nchini waone namna nzuri ya kushirikiana nao ili kusaidia kuwakwamua kiuchumi kwani itakuwa ndio fursa ya jamii nayo kuinuka kimaendeleo.

 “Kwa kweli ni muhimu viongozi wa ngazi mbalimbali kuona namna nzuri ya kushirikiana na wajasiriamali kwa kuona namna ya kuwasaidia kwa lengo la wao waweze kufikia malengo yao kwani hata Rais Dkt John Magufuli amekuwa akishirikiana nao hivyo waige mfano huo “Alisema

“Kwa hapa Muheza mimi nimshukuru Mkurugenzi wa Halmashauri ya  Muheza kwani amekuwa na ushirikiana mkubwa kwa wadau mbalimbali ambao wanafika kwake na hii itasaidia kuwarakisha gurudumu la maendeleo yawananchi”Alisema

Kutokana na hali hiyo alilazimika kuwaunganisha na SIDO Mkoa wa Tanga na siku ya wanawake duniani wakaona wazindue mafunzo ya wajasiiriamali kwa wanawake wa Tadaha Women Products kwa wiki moja ambayo yatakuwachachu kubwa kwao kuweza kufikia malengo yao

Awali akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo ,Amiri Msuya kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Halamshauri ya Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga aliipongeza Taasisi hiyo kwa kutoa mafunzo hayo huku akieleza kwamba ni matumaini yatakuwa chachu kubwa kwa walengwa kuweza kufikia malengo yenu kwa kutumia fusa zinazowazunguka kwa ajili ya kuinua vipato vyetu na hatimaye kuboresha maisha yao kwa kufauata sheria za nchi zilkizokwe.

Alisema kwa sababu Kwenye kumkomboa mwanake wa kitanzania sio jukumu la serikali pekee bali pia wahisani kama DIWO kwa sababu lengo la serikali ni kumfanya mwanamke aweze kujitegemea na kuondokana na hali ya utegemezi.

Alisema jambo hilo ambalo limekwisha kuanza kuondoka kwa wanawake kwa sababu wamekwisha kuanza kujitambua na wamekuwa wakitafuta fedha kuliko wanaume na kuondoa ile dhana ya kwamba wao wamekuwa ni tegemezikwa kila kitu kwenye jamii.

“Wanawake dhana ya kujitegemea tuitumie kwa vitendo kwa sababu akifundishwa na mwamnanke na mwamaume mwanamke anauwezo wa kuelewa haraka zaidi kuliko mwaume kwa asilimia 75 ila wanasahau haraka kuliko wanaume hivyo tumieni nafasi hii ya kuelewa kwenu kwa harakakuwasaidie kubadilisha mfumo wa maisha yenu”Alisema .
 
Kaimu Mkurugennzi huyo alisema kwamba ili wazalishe sabuni kuna kemikali ambazo zinaweza kutumika hivyo washiriki wa mafunzo wakayatumie kwa vitendo ujuzi huo ambao wameupata ili  kuzalishiakipato na mchango kwao na serikali.

“Lakini siku ya mwanamke dunia kama leo ni mwanzo mpya wa kumfanya mwanamke aiende kwenye ulimwengu bora kuliko ambako alikuwa ametoka hivyo mafunzo hayo yatawasaidia kuweza kufikia ndoto zenu za kujikwamua “Alisema Kaimu Mkurugenzi huyo.

Naye kwa upande wake Katibu wa Kikundi cha Tadaha Women Products bi Magreth Mngazija alisema kwamba mafunzo hayo yatawasaidia sana maana wanaona walipotoka na wanapokwenda yatakuwa chachu kubwa kwao kufikia malengo yao.

Alisema pia elimu hiyo walioipata wataitumia kama chachu ya kuweza kujikwamua kiuchumi kwa kutengeneza bidhaa bora ikiwemo kuwasaidia wana vikundi vyengine vilivyopo kwenye maeneo yao kwa kuwapatia ujuzihuo



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post