Wezi wavunja kanisani na kuiba vifaa vya ibada |Shamteeblog.

Na Amiri Kilagalila,Njombe

Watu wasiojulikana wameingia Kanisa la Parokia ya Mt. Augustino Wanging'ombe Jimbo Katoliki la Njombe kwa kupitia dirishani (kwa kulivunja) na kuiba vitu mbali mbali vinavyotumika kwa ajili ya maadhimisho ya misa takatifu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Askofu na Mkurugenzi wa
Idara ya Habari na Mawasiliano Jimbo la Njombe Pd. Innocent Chaula.Imeeleza kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Jumanne 09 Machi 202.

Amesema vifaa vilivyoibwa ni pamoja na.

1. Custodium yenye Ekaristi ya Mwonyesho ndani.
2. Monstrance
3. Kalisi (4)
4. Ciboria (3)
5. Patena (1)
6. Chombo cha kuwekea ubani (1)
7. Surplice (1)

Ambapo vyombo hivyo hutumika kwa ajili ya maadhimisho ya Misa Takatifu na Ibada za Kuabudu Ekaristi Takatifu.

Ameongeza kuwa wezi hao wamechagua vitu vyenye rangi ya dhahabu tu, vile vilivyokuwa na rangi ya shaba vimeachwa.

Aidha amesema walifungua Tabernakulo na kuchukua ciborium yenye Ekaristi Takatifu. Ekaristi Takatifu waliimwaga kwenye meza ya sakrastia na wao wakaondoka na Ciborium.

Ametoa rai kwa jamii  kusali na kuombea tukio hilo ili vitu vyote viweze kupatikana na kukumbusha kuimarisha ulinzi wa makanisa na maeneo yote ya parokia na taasisi.

Vile vile amekumbusha kumfariji Paroko wa W'ng'ombe Pd. Renatus Mwalongo katika kipindi hiki kigumu.

Katika hatua nyingine akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wetu ili kuthibitisha tukio hilo amesema ni kweli wizi huo umetokea na uongozi wa Jimbo umefika sehemu ya tukio na kuthibitisha hili.huku taratibu za kuwatafuta wezi hao zinaendelea kwa kushirikiana na Polisi.







 


By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post