UONGOZI wa kampuni ya kubashiri matokeo ya Meridian Bet imetoa mkono wa faraja kwenye kituo cha kulea watoto yatima cha Mama wa Huruma kilichopo Madale, Dar es Salaam.
Afisa Huduma wa jamii wa Meridian Bet, Amani Maeda aliyeambatana na meneja mwendeshaji, Corrie Borman wamesema kampuni yao imeguswa na changamoto ya kituo hicho na kujitoa kukisaidia.
Alisema kwa namna Meridian Bet inavyoguswa na jamii, wameona kusaidia kituo hicho ni wajibu wao kama ambavyo wamekuwa wakifanya kwa jamii yenye uhitaji.
"Tumetoa cement, gypsum poda na pesa kidogo kama kianzio katika ukarabati wa jengo ambalo linatumiwa kama bweni na watoto hawa ambalo tumeelezwa linatumika lakini halijakamilika kujengwa, pia tumetoa vyakula kama sukari, unga, mchele, mafuta na sabuni."
Sister wa kituo hicho, Christina Christopher aliishukuru Meridian Bet na kueleza kwamba wamewapa faraja kipindi hiki ambacho wako kwenye changamoto ya watoto kulala kwenye jengo ambalo halijakamilika.
Alisema baadhi ya watoto wanalazimika kulala katika jengo hilo ili kupunguza msongomano kwenye jengo la awali kwa lengo la kuchukua tahadhari ya janga la corona kwa kupunguza msongamano kwenye jengo la awali.
By Mpekuzi
Post a Comment