MWALIMU APONGEZA UTEUZI WA DK BASHIRU |Shamteeblog.

NA DENIS MLOWE,IRINGA

 MWENYEKITI  wa Jukwaa la Walimu Wazalendo mkoa wa Iringa, Mwalimu Marysina Ngowi  amepongeza uteuzi  wa aliyekuwa katibu mkuu wa CCM Taifa Dk. Bashiru Ally kuwa katibu mkuu Kiongozi uliofanywa na Rais John Magufuli kuwa ni mtu sahihi ndani ya taifa kutokana na kuwa mwadilifu na mtu makini aliyechangia kwa kiasi kikubwa CCM kuwa chama bora na makini nchini.

 Marysina Ngowi ambaye pia ni afisa utamaduni wa manispaa ya Iringa na kada kindakindaki wa chama cha Mapinduzi alisema kuwa uteuzi huo umekuja katika wakati mwafaka na mtu sahihi kwa sasa nchini kutokana na utendaji kazi wake usio na mashaka wakati yuko ndani ya chama na alipokuwa mtumishi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam kama mhadhiri.

 Alisema kuwa uadilifu alionao katibu mkuu kiongozi Dk. Bashiru hauna mashaka kwa mtu yoyote anayefatilia siasa nchini hivyo kitendo cha kuchaguliwa kuwa katika mkuu kiongozi ni kiasi gani Rais wa Tanzania John Magufuli amefanikiwa kuweza kuziba pengo la aliyekuwa katibu mkuu kiongozi Marehemu Balozi John Kijazi.

 Marysina ambaye pia ni balozi wa hiari wa kupinga ukatili wa kijinsia kwa watoto na wanawake kupitia kampeni inayoitwa ‘don’t touch hapa kwangu’ alisema kuwa Dk. Bashiru amefanya mengi wakati alipokuwa katibu mkuu wa ccm ikiwemo ushujaa wake wa kusimamia kamati iliyosaidia kuhakiki mali zote za CCM na kukifanya CCM kujiendesha kwa mali inazomiliki.

 Aliongeza kuwa elimu aliyonayo Dk Bashiru ni msaada mkubwa katika nchi  ya Tanzania na uhakika mkubwa wa kumsaidia Rais Magufuli katika utendaji kazi wake mkubwa wa kuwaletea maendeleo watanzania ambao wana imani kubwa kwake.

 Alisema pasipo shaka kuwa mmoja wa viongozi waliojipambanua kuwa hawana kashfa na mwenye nidhamu ya kazi na maono kuhusu nini kinatakiwa kufanywa na uwezo wa kujenga hoja alionao Dk. Bashiru umemfanya kuwa kiongozi wa kipekee alipokuwa ndani ya chama hivyo hali hiyo ataitumia kipindi ambacho amekuwa Katibu Mkuu Kiongozi wa serikali.

 “Dk. Bashiru ni mtu sahihi kabisa kwani amekuwa akisimamia misingi na utendaji bora wa kazi hivyo tutegemee makubwa katika uongozi wake kama katibu mkuu kiongozi na utamu zaidi alisomea utawala wa umma hivyo hongera  kwake rais kwa kumwona Dk. Bashiru katika nafasi hiyo ambayo mtu makini kama alivyokuwa marehemu Kijazi anahitajika katika kusukuma utendaji kazi wa umma” alisema

 Aidha aliwabeza wote ambao wamekuwa wakikosoa uteuzi huo kuwa Rais hajafata sheria katika uteuzi na kuwataka kuwafahamu kuwa Dk. Bashiru alikuwa mtumishi wa umma kupitia chuo kikuu cha Dar es salaam na kuteuliwa kwake kuwa balozi ni kutokana na sheria na mamlaka aliyonayo rais kuruhusu kufanya hivyo.

Marysina Ngowi akizungumza



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post