Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa(ARPP), Sisty Nyahoza (wa kwanza kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa kitaifa wa Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT – Wazalendo) mara baada ya kumaliza mafunzo ya namna ya kujaza fomu za marejesho ya gharama za uchaguzi yaliyofanyika mapema hivi karibuni katika ukumbi wa Samwel Sitta Ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia waliokaa ni Mkuu wa Idara ya Uchaguzi na Ruzuku, Bi. Hollo Kazi, Katibu Mkuu wa ACT- Wazalendo, Ado Shaibu na Kaimu Mwenyekti wa chama hicho, Dorothy Semu. (Picha na ORPP) Katibu Mkuu wa Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT – Wazalendo),Bw. Ado Shaibu akichangia mada wakati wa mafunzo ya namna ya kujaza fomu za Marejesho ya Gharama za Uchaguzi kwa Viongozi wa Kitaifa wa Chama cha ACT – Wazalendo mapemaa hivi karibuni katika ukumbi wa Samwel Sita Ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa chama hicho, Bi. Dorothy Semu. Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT – Wazalendo), Bi. Dorothy Semu akipitia nyaraka wakati wa mafunzo ya namna ya kujaza fomu za Marejesho ya Gharama za Uchaguzi kwa Viongozi wa Kitaifa wa Chama cha ACT – Wazalendo mapemaa hivi karibuni katika ukumbi wa Samwel Sita Ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam.Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa chama hicho Bw. Ado Shaibu. Mkuu wa Sehemu ya Usajili wa Vyama vya Siasa toka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP) na Mwenyekiti wa mafunzo, Bw. Muhidin Mapeyo akifungua mafunzo ya namna ya kujaza fomu za Marejesho ya Gharama za Uchaguzi kwa Viongozi wa Kitaifa wa Chama cha ACT – Wazalendo mapemaa hivi karibuni katika ukumbi wa Samwel Sita Ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam. Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa(ARPP), Sisty Nyahoza akiwasilisha mada mbele ya viongozi wa Chama cha ACT – Wazalendo wakati wa mafunzo ya namna ya kujaza fomu za marejesho ya gharama za uchaguzi mapema hivi karibuni katika ukumbi wa Samwel Sitta zilizopo Ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam.
By Mpekuzi
Post a Comment