Golikipa wa Simba SC, Aishi Manula amesema yupo tayari kwa maamuzi ya timu yake ya Simba SC kuamua yeye kubaki au kuuzwa klabuni hapo.
Manula amehusishwa kusajiliwa na Klabu ya El Merreikh ya Sudan 🇸🇩 na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini 🇿🇦 licha kuwa na mkataba na Wekundu wa Msimbazi.
Kwenye mahojiano yake na kituo cha runinga cha Azam TV baada ya mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Aishi amesema yupo tayari kwa changamoto ndani au nje ya nchi kwa msimu huu au msimu ujao wa mashindano.
“Inafahamika Mchezaji akiwa na mkataba na timu fulani, kama kuna Klabu inataka kumsajili basi inafika kwa timu ambayo Mchezaji huyo ana mkataba nayo ana ana itumikia kwa wakati huo”, amesema Manula.
By Mpekuzi
Post a Comment