Nyota saba wa kikosi cha Simba leo wanatarajiwa kuukosa mchezo wa wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar utakaochezwa Uwanja wa Kaitaba majira ya saa 10:00 jioni.
Ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Didier Gomes ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Kagera Sugar inayonolewa na Kocha Mkuu, Francis Baraza.
Miongoni mwa nyota hao ambao watakawakosa Kagera Sugar ni pamoja na Francis Kahata ambaye yeye hayupo kwenye hesabu za mechi za ligi na badala yake yupo kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika na Simba imetinga hatua ya robo fainali.
Bernard Morrison kiungo huyu mchetuaji ana kadi tatu za njano ambazo alizipata kwenye mechi tatu tofauti ambapo ya tatu ilikamilika wakati ubao ukisoma Mwadui 0-1 Simba, Uwanja wa Kambarage.
Gadiel Michael, Said Ndemla,Miraji Athuman, Ibrahim Ajibu, Ally Salim nyota hawa watakosekana kwa kuwa hawana 'match fitnes' pia kwenye mpango wa Gomes imekuwa ngumu kwao kupenya kikosi cha kwanza.
Kwenye mchezo uliopita dhidi ya Mwadui FC ni Morrison pekee alianzia benchi huku hao wengine majina yao yakiwa adimu kuonekana kwenye kikosi cha kwanza.
Hivi karibuni Gomes alisema kuwa ushindani wa namba ni mkubwa ndani ya kikosi hicho hivyo wachezaji wanapaswa kupambana zaidi.
from Author
Post a Comment