MTAYARISHAJI maarufu wa kazi za muziki Bongo, P Funk Majani ambaye ni Baba wa Paula amesema mambo anayoendelea kuyafanya mtoto wake huyo pamoja na mzazi mwenzake Kajala (ambaye ni mama wa Paula) yanaidharirisha familia ya P Funk.
Haya yamekuja baada ya kusambaa kwa video zikimwonyesha Paula akiwa kwenye pozi za kimahaba na msanii wa WCB, Rayvanny lakini baadaye tena kukaibuka picha mitandaoni na chatting zinazodaiwa kuwa ni za msanii Harmonize akimtongoza Paula licha ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mama wa binti huyo ambaye ni Kajala.
Akizungumza kupitia Kipindi cha XXL cha Clouds FM, Majani amesema; “Nilishawaambia tangu mwaka jana kwamba Mimi nilishajitoa, nilishanyoosha mikono kwa Paula, mtoto anatafuta laana alishaniambia wewe sio Baba yangu, Kajala sio familia yangu nilifanya uamuzi mbaya kuzaa na mtu ambaye sio sahihi kuwa mama, yanayoendelea hayanihusu.
“Mimi kwa sasa nina familia yangu ambayo nina-play kama Baba na wanavyoendelea kufanya vinaathiri mpaka familia yangu hii nyingine kwa sababu inahusishwa nao, uchafu wao (Kajala na Paula) una reflect kwa hawa wengine, wamekosea wanatuvunjia heshima.
“Maisha sio Instagram, vitu vya Kifamilia mnatatua Kifamilia naona Instagram wanasema ‘toa tamko’, nitoe tamko Instagram? Masuala ya kuvujisha mavideo sio sahihi, ugomvi wa kimapenzi kwa nini muweke mtandaoni, matatizo ya Familia huweki mtandaoni, jiheshimu utaheshimiwa,” Producer P Funk Majani, Baba wa Paula.
from Author
Post a Comment