Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo, jana amekutana na kufanya mazungumzo na Madereva takribani 500 wa Kiwanda cha Dangote Mkoani Mtwara, waliokuwa wamegoma kwa siku 12, baada ya majadiliano Uongozi wa Kiwanda hicho umekubali kuwalipa stahiki zao ikiwemo mishahara na kuahidi kurejea kazini leo.
"Tutasimamia kuhakikisha Kiwanda cha Dangote kinaendelea na uzalishaji na kupata faida, lakini kinatekeleza wajibu wake kwa watu wetu, hatutaki watanzania wanyanyasike katika Nchi yao” - Kitila Mkumbo
“Nchi hii ni huru, tutalinda haki za Madereva, nanyi pia mtulindie heshima yetu kwa Mwekezaji kwa kuwa Waaminifu” - Kitila Mkumbo
from Author
Post a Comment