TISA WAHITIMU PROGRAMU YA MFUNZO KWA WAKUFUNZI(TOT) KATIKA KOZI YA HUDUMA NDOGO YA BIMA ...FSDT YATAJA FAIDA |Shamteeblog.

Na Said Mwishehe, Michuzi TV.


WAHITIMU tisa wamehitimu mafunzo ya programu ya mafunzo kwa wakufunzi(TOT) katika kozi ya huduma ndogo ya bima ikiwa ni moja ya mkakati wa kuendeleza ujuzi na uwezo katka sekta ya huduma ndogo za bima ili kuboresha bidhaa na utoaji wake kwa ustawi wa Watanzania wenye kipato cha chini.
Uratibu wa kufanikisha mafunzo hayo umefanywa na Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha Tanzania(FSDT) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania(TIRA),Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM),Taasisi ya Bima Tanzania(IIT) na Kikosi kazi cha Wataalamu(TWG) ambao wote hao walikuepo wakati wa mahafali ya wahitimu hao yaliyofanyika katika ofisi za FSDT jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa mahafali hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha Tanzania(FSDT) Sosthebes Kiwia amesema mafunzo hayo ni maalumu ya wakufunzi wa bima hapa Tanzania , wahitimu hao tisa wamebobea katika kufundisha watu wengine katika bima hasa zinazohusu watu wa kipato cha chini , na wale ambao wanahitaji zaidi kujikinga na majanga mbalimbali kwa mfano wanawake,vijana na wakulima na waishio vijijini.

"Bima kama hizi zinaweza kuhusisha bima za afya na bima za kilimo, na mafunzo haya yanalenga kuhakikisha watu wanafaidika na huduma za bima, hawa ambao wanahitimu wanaweza kuwa chachu ya kutosha kuongeza kasi ya ukuaji wa bima hapa nchini na lengo lingine ni kuhakikisha sekta ya bima linakuwa na tija zaidi katika tasnia ya fedha kwa ujumla lakini katika tasnia ya kilimo, biashara na maeneo ya jamii.

"Hawa wahitimu wako tisa lakini kama nilivyosema wao ni chachu katika kutoa mwangaza wa namna gani sheria na kanuni katika soko la bima ziwe bora zaidi na watakuwa na mwangaza katika soko zima ili kuashiria na kubobresha miundombinu ya usambazaji wa huduma za bima.Wote  tunafahamu  ubunifu ni kitu muhimu sana, hawa wahitimu wamepata mafunzo kuhusu ubunifu na ubunifu huu utakuwa na tija zaidi pale watakapounganisha na mifumo ya teknolojia,"amesema.

Ameongeza  watu wengi ambao wanatumia huduma za bima sasa hivi wanapata kupitia simu za mkononi mkwa hiyo wanaamini kwamba hayo mafunzo yaliyotolewa kwa wahitimu hao tisa,wataweza kuwafikia watu wengi zaidi ambao wanajishughulisha na usambazaji wa bima wakiwemo mawakala na itakuwa ni nafasi kubwa kwao kuleta mabadiliko yanayoleta tija katika jamii yetu.

Amefafanua lengo kubwa ni kuhakikisha jamii ya Watanzania wanajikinga na majanga na njia mojawapo ni kutumia bima."Haya mafunzo yanalenga kuleta hayo maendeleo hapa nchini na kuhusu hali ilivyo kwa sasa katika sekta ya bima, hapa Tanzania bado kuna changamoto watu wengi hawatumii huduma za bima hasa zinazotolewa na taasisi rasmi, bima kubwa kabisa inayotumika ni bima ya afya na utafiti wa mwaka mwaka 2017 ni asilimia 16 ya watanzania wanaotumia bima za afya.

"Lakini  bima nyinyine kama za magari, kilimo nyumba, ziko chini ya asilimia mbili, kwa takwimu hizi inaonesha kuna fursa kubwa sana ya kuweza kuleta ubunifu na kuchochea ukuaji wa huduma za bima.Hata mchango wa sekta ya bima katika tasnia ya fedha bado mdogo, mchango wa bima katika ukuaji wa uchumi bado ni mdogo kulinga na mpango wa maendeleo katika sekta ya fedha wa miaka 10 kuanzia mwaka 2020 hadi mwaka 2020 unaazimia mchango wa bima kufikia asilimia tano,"amesema.

Amesisitiza sasa hiyo ni kazi kubwa, hivyo kunahitajika mafunzo yenye weledi wa hali ya juu , ujuzi wa hali ya juu na sio tu kwa hao wahitimu tisa bali kwa wote wanaotoa huduma za bima hasa  zinazowalenga wanawake,vijana na wakulima na waishio vijijini. Kuhusu miundombinu bima ,Kiwia  amesema kuna changamoto ya kutumia miundombinu  mbalimbali ya kusambaza huduma za bima.


"Mawakala wa huduma za bima wa kampuni ni wachache sana ,hawazidi hata 1000 kwa hiyo ukiangalia ukubwa wananchi hasa idadi ya watu watu wote ni kama milioni 60 hivi, kweli mawala 1000 hawatoshi lakini bahati nzuri teknolojia imesaidia kupatika kwa mawakala wengi kupitia kampuni za simu,"amesema.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Sheria wa Mamlaka ya Bima Tanzania Emiry Kiria amesema kwa ujumla mamlaka yao imeundwa kisheria na kimsingi ina majukumu mengi yakiwemo ya kuandikisha kampuni za bima na madalali wa bima, mawakala na watu wote wanaopenda kujihusisha na biashara hiyo, lakini zaidi baada ya kuwaandikisha wanawasimamia ili kufuata sheria za bima , taratibu na kanuni.

"Kwa hiyo tumealikwa hapa kuhudhuria sherehe za kumaliza elimu ya watu wa bima, lakini kuja kwetu tumeona ni nafasi kuja kujifunza jinsi ambavyo hawa watu walichokisoma na umuhimu wa hicho walichokisoma katika soko la bima , kwa ujumla kuna upungufu mkubwa wa watalaam kwenye soko la bima, bado hatuna watu wengi hasa ambao wamesoma mambo ya bima kwa kiwango kikubwa,

"Nasema hatuna wengi kwasababu hata ukiangalia waliohitimu leo ni tisa tu ambao ni wachache kwa muda wa miaka minne waliokuwa darasani lakini hawa ni walimu wa kwenda kufundisha wengine , ni walimu wa walimu kwa hiyo tunategema watakapokwenda kwenye soko watakuwa chachu, kikubwa tunachosisitiza ni kuendelea kutolewa kwa mafunzo ya bima.Aidha Mkuu wa Kitengo cha Bima na Ulinzi wa Watumiaji Kemibaro Omuteku, ameongeza wanawapongeza wakufunzi tisa ambao wamefuzu kama wakufunzi wa kozi ya msingi ya huduma ndogo za bima.

Wakati Mwakilishi wa Chama cha Makampuni ya Bima Tanzania(ATI) na Kikosi Kazi cha Utaalamu waTasnia ya Bima Ndogo(TWG),Neema Kaaya,amesema vyombo vyote viwili vinaunga mkono mpango wa programu ya Mafunzo ya Wakufunzi(ToT)kwani unaendana na malengo  makuu ya sekta ya bima nchini na utekelezaji wake

Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha Tanzania(FSDT) Sosthebes Kiwia akizungumza wakati wa mahafali hayo ya wahitimu tisa wa mafunzo ya programu ya mafunzo kwa wakufunzi(TOT).Mahafali hayo yamefanyika katika ofisi za FSDT zilizopo jijini Dar es Salaam.Wakikilishi kutoka Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha Tanzania(FSDT),Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania(TIRA),Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM),Taasisi ya Bima Tanzania(IIT) na Kikosi kazi cha Wataalamu(TWG) wakiwa katika mahafali ya wahitimu tisa waliohitimu mafunzo ya programu ya mafunzo kwa wakufunzi(TOT).
Wahitimu wa mafunzo ya programu ya mafunzo kwa wakufunzi(TOT) wakiwa kwenye mahafali yao baada ya kuhitimu baada ya kusoma kwa kipindi cha miaka minne.
 


By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post