Ajali ya Ndege ya Kijeshi Marekani |Shamteeblog.

 


Rubani mmoja ameripotiwa kufariki kutokana na ajali ya ndege ya kijeshi iliyotokea ilipokuwa ikipaa kutoka kituo cha Jeshi la Anga cha Nellis katika jimbo la Nevada nchini Marekani.

Ndege hiyo ya kijeshi, ambayo ilipaa kutoka kituo cha Jeshi la Anga cha Nellis, ilianguka hapo jana mwendo wa saa 14:30 kwa sababu isiyojulikana.


Kikosi cha jeshi la Anga cha Nellis kilitangaza kuwa ndege hiyo ilikuwa inamilikiwa na Draken US, kampuni ya Florida iliyopewa kandarasi ya kutoa msaada wa anga, na rubani wake ambaye hakufahamika alifariki.


Wakati huo huo, Draken US ilitoa maelezo juu ya ajali hiyo kwa kusema,


"Tunafanya kazi kwa karibu na maafisa wa shirikisho, serikali na utawala wa mitaa. Vile vile Draken US inashirikiana na mashirika ya uchunguzi ili kutambua chanzo kilichosababisha ajali hii mbaya."



from Author

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post