BENKI YA TAIFA YA BIASHARA YATOA MIFUKO 500 SARUJI UJENZI WA MADARASA KIGOMA |Shamteeblog.


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC,  Theobald Sabi (kati) akimsikiliza kwa makini Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Rashid Mchatta (kulia) baada ya hafla fupi ya kukabidhi mifuko 500 ya saruji kwa Mkoa wa Kigoma, kushoto ni Meneja wa Wateja Wadogo na wa Kati, Elibariki Masuke.
Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC,  William Kalaghe akiongea machache wakati wa kukabisdi wa msaada wa mifuko 500 ya saruji kwa serikali ya Mkoa wa Kigoma ili kusaidia kwenye ujenzi wa madarasa mkoani humo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC, Theobald Sabi (wanne kulia) akikabidhi msaada wa mifuko mia tano 500 ya saruji yenye thamani ya TSHS 10,500,000 kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali kwenye sekta ya elimu kwaajili ya ujenzi wa madarasa katika shule mkoani humo. Mifuko hiyo ilipokelewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Rashid Mchatta kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa,Thobias Adengenye. Wengine katika picha ni Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Kigoma.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NBC wakiteta jambo kwa pamoja wakati wa kukabidhi msaada wa mifuko 500 ya saruji kwa serikali ya Mkoa wa Kigoma ili kusaidia juhudi za mkoa huo katika ujenzi wa madarasa.


BENKI ya Taifa ya Biashara NBC imekabidhi mifuko 500 ya saruji kwa Mkoa wa Kigoma kusaidia juhudi za serikali za ujenzi wa madarasa mkoani humo.

 Katibu Mtendaji wa Mkoa wa Kigoma,  Rashid Mchata akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Thobias Andengeye pamoja na kuishukuru Benki ya NBC alisema kuwa kuna uhaba mkubwa wa madarasa kutokana na muamko wa wazazi wa Kigoma kupeleka watoto shule kufuatia maamuzi ya serikali kutoa elimu bure. 

“Tunategemea wanafunzi wapatao 40,771 kuhitimu darasa la saba na kuingia kidato cha kwanza mwaka 2022 kuepelekea uhitaji wa  madarasa ziaidi ya 1,010 huku mkoa wetu ukiwa na madarasa 405, hivyo mchango wa Benki ya NBC wa mifuko 500 ya saruji utaisaidia kusukuma malengo serikali yetu ya mkoa kukamilisha ujenzi wa madarasa zaidi ya 605.” Alisema Mchata.

Akiongea baada ya kukabidhi msaada huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi alisema kuwa msaada huo wa mifuko 500 ya saruji yenye thamani ya TSHS 10,500,000 ni kielelezo kidogo tu cha dhamira ya dhati ya kurudisha kwa jamii kiasi cha faida inayopatikana kutokana na kuwahudumia Watanzania. 

“Sera yetu ya kurudisha sehemu ya faida kwa jamii inayotuzunguka inaangalia maeneo ya elimu, afya na ustawi wa jamii kama nguzo kuu. Ni kweli mchango wetu huu haitamaliza changamoto ya vyumba vya madarasa lakini nia yetu kama taasisi ya biashara ni kuendelea kurudisha sehemu ya faida kwa jamii hivyo tutaendelea kushirikiana na serikali ya mkoa katika juhudi mbali mbali za kutatua changamoto katika jamii, huu si mwanzo bali ni muendelezo.” Alisema Sabi.

Aidha kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu,  Joseph K Rwiza ambaye wilaya yake ni moja kati wa wilaya nufaika wa msaada huo ameishukuru Benki ya NBC kwa mchango wao. Pia alieleza kwamba serikali ya wilaya yake itaunganisha nguvu za bajeti pamoja wananchi na wadau wengine kuhakikisha kwamba changamoto ya uhaba wa madarasa inakuwa historia katika wilaya yake.



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post