JESHI la Polisi Mkoa wa Songwe, limeanza uchunguzi tuhuma za Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Samuel Jeremiah, kuhusu kumtishia kumuua Mbunge wa Songwe (CCM), Philip Mulugo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, George Kyando, akizungumza katika mahojiano na Gazeti la Nipashe jana, alisema jeshi hilo limeanza uchunguzi na tayari limeshamwita na kumhoji Jeremiah.
“DC anahojiwa na yule aliyetuhumu (mbunge) naye anahojiwa. Hakuna aliyeshtaki isipokuwa taarifa kama hii usisubiri mpaka mtu ashtaki. Tuhuma kama hizi kwa viongozi kama hawa wa serikali lazima jeshi lichunguze ili sheria ichukue mkondo wake,” alisema.
Kamanda Kyando alisema baada ya uchunguzi kukamilika na ikionekana kuna jinai sheria itachukua mkondo wake na kama ikibainika hakuna, hatua nyingine zitachukuliwa ili kumaliza suala hilo
CREDIT: NIPASHE
from Author
Post a Comment