DC Msafiri apiga marufuku watoto chini ya miaka mitano kulipia matibabu |Shamteeblog.


 Amiri Kilagalila na Blighither Nyoni

Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri ameagiza kituo cha afya Makambako kuacha mara moja kuwatoza fedha watoto chini ya miaka mitano kwa ajili ya matibabu kwa kuwa ni kinyume na sera ya Afya.

Akizungumza na kituo hiki kufuatia malalamiko ya baadhi ya wanachi wa halmashauri ya mji wa makambako kulalamikia kutozwa shilingi 4000 kwa ajili ya matibabu ya watoto walio na umri chini ya miaka mitano wanapohitaji kumuona daktari, Mkuu wa wilaya amesema Sera ya afya inataka mtoto chini ya miaka mitano kutibiwa bure hivyo wanapaswa kutekelezaa sera hiyo kikamilifu.

“Hatua hizo za makamabko siziungi mkono hata kidogo,na pia nazikataa kwasababu walishawahi kuja kuniambia kwamba wamefuta basi wasirudie na sio sahihi kumchukua mtoto na kumwambia utakuja kwa rufaa”alisema Ruth Msafiri

Aidha Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Makambako Hanana Mfikwa amekiri kuwepo kwa tatizo hilo kutokana na mkanganyiko uliojitokeza baada ya ujio wa Naibu waziri Tamisemi  Dokta Festo Dugange pamoja na muongozo wa serikali hivyo wameuondoa utaratibu wa kulipia na sasa watoto chini ya miaka mitano,wajawazito na wazee wasiojiweza wanatibiwa bure.

“Ni kiri kwamba tatizo hili tulifuatilia tuliona lilikuepo,kwa hiyo watoto,wajawazito na wazee hawataendelea kutozwa na mpaka sasa zoezi hilo limesimamiswa kwa watoto kuanzia mwaka 0 mpaka 5 wanatakiwa wapate huduma hii ya afya bure  lakini wazazi wazingatie kwenda na kadi”alisema Hanana Mfikwa

Hata hivyo mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Makambako Paul Malala amewataka wananchi kuzitumia zahanati ambazo zimejengwa katika kata mbalimbali  badala ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya katika kituo cha afya makambako.

“Tuna ngazi mbali mbali za upataji wa huduma za afya kuanzia zahanati,kituo cha afya na kuendelea na kilichokuwa kinafanyika ni kuwaelewesha wazazi tu namna ya kupata huduma za afya”alisema Malala

Nao baadi ya wananchi mjini makambako wameishukuru serikali kwa kuwarejeshea utaratibu wa matibabu bure kwa watoto  walio chini ya umri wa miaka mitano kwa kuwa imewapunguzia mzigo wa wazazi kuchangia gharama za matibabu.

Sera ya Afya ya mwaka 2007 hapa nchini inataka huduma za Afya kwa wazee wasiojiweza, wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano kupata huduma bure.

 

Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri



By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post