Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini akimkabidhi waziri wa katiba na sheria Geofrey Mizengo Pinda simu janja tayari kwa kwenda kuanza kazi ya kusajili watoto chini ya miaka mitano.
Na Woinde Shizza , Michuzi Tv Arusha
KAMPUNI ya mtandao wasimu Tigo Tanzania imechangangia simu janja 1350 yenye thamani ya milioni 169 kwa mkoa wa Arusha na Manyara ili kuweza kuhakikisha zaidi ya watoto laki 6 wanasajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa.
Hayo yameelezwa na mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini Henry Kinabo wakati akiongea katika uzinduzi wa wa mpango wa usajili watoto wa umri chini ya miaka mitano kwa mikoa ya Arusha na Manyara ambapo alisema kuwa Tigo inatambua kuwa nyaraka za awali za utambulisho wa mtoto ni cheri Cha kuzaliwa hivyo wazazi na walezi wajitokeze kwa wingi kuwapatia wao haki yao.
Alieleza kuwa Tigo wamefanikiwa kuonesha umuhimu wa matumizi ya teknolojia katika zoezi hilo na wameendelea kuwekeza hivyo jambo hilo lipewe umuhimu ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa katika kata zote na vituo vya kutolea huduma ya mama na mtoto vinavyotakiwa kutekeleza zoezi hilo.
Aidha alifafanua kuwa simu hizo zimepewa kipaumbele katika minara yote ya Tigo ambapo suala la mtaandao katika ufanyaji wa zoezi hilo halitakuwa na changamoto yoyote.
Kwa upande wake Naibu waziri wa katiba na sheria Geofrey Mizengo Pinda wakati wa kuzindua zoezi hili alitoa shukrani kwa wadau wate wa maendeleo waliosaidia zoezi hilo wakiwemo Tigo Tanzania kwa lkuendeleza muhimilihuo kwani wamekuwa chachu kubwa ya kuhakikisha mpango huo unaendelea na kufanikiwa.
Naye mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akimuwakilisha mkuu wamkoa wa Arusha Iddi Kimanta katika uzinduzi huo alisema kuwa fedha walizozitoa wadau hao na kuziweka katika zoezi hilo lazima zikatoe matokeo chanya kwa kuhakikisha watoto wanasajiliwa kwa asilimia 100.
By Mpekuzi
Post a Comment