Na Muhammed Khamis,TAMWA-ZNZ
MKURUGENZI wa Chama cha Waandishiwa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA, ZNZ) Dkt Mzuri Issa Ally amewataka wazazi na walezi kuhakisha wanaongeza ulinzi kwa watoto wao katika kipindi hichi cha sikukuu ya Eidl fitr kwa lengo la kuwalinda na matukio mbali mbali yakiwemo ya kubakwa, kulawitiwa na hata kupotea kusikojuulikana .
Alisema licha ya siku hio ni furaha kwa wananchi wote lakin wasingeuze furaha hio kuwa sehemu ya kuwaacha watoto wakitembea ovyo mitaani kwani wapo baadhi ya watu wenye nia ovu wanaweza kusababisha madhara makubwa.
Itakumbukwa kuwa katika miaka iliyopita kipindi kama hichi cha sikukuu huripotiwa kesi nyingi za udhalilishaji kwa wastani wa kesi tano kwa siku, ambapo watoto waliopo chini ya umri wa miaka 18 hutoroshwa ama kubakwa.
Aidha alieleza kuwa wakati tukisubiri saa chache kuingia kwa siku hio ya furaha kubwa mitandao ya kupambana na udhalilishaji imeleza kuwa kutoka mwezi disemba hadi machi wameibua na kufanyika kazi matukio ya udhalilishaji yapatayo 76 ambapo kwa Unguja ni 44 na Pemba 32 hali ambayo inaonesha kuwa bado matukiohayo yapo na yanapaswa kutazwa kwa umakini mkubwa.
"Kikawada kuna makundi ya watoto huonekana kuranda mitaani kipindi chote cha skukuu bila ya kuwa na ulinzi wakiomba mkono wa eid mazingira mabyo tunaamini sisi baada ya watu wanaweza kutumia kama sehemu ya fursa ya kufanya uovu wao." Aliongezea.
Baadhi ya wakati watoto kwa kutokujua hujikuta wanaingia katika nyumba ambazo wanaishi watu wasiokua wema na huwarubuni kwa kuwapa skukuu na hatimae huwafanyia vitendo viovu jambo ambalo linarudisha nyuma nguvu kazi ya Taifa.
Sambamba na hoyo Mkurugenzi huyo alitoa wito kwa jeshi la polisi kuongeza kasi ya ulinzi zaidi katika maeneo mbali mbali ya viwanja vya kufurahishia watoto pamoja na kukagua magari yanayotoa huduma za abiria katika kipindi chote cha sikukuu.
By Mpekuzi
Post a Comment