Na Mwandishi wetu, Michuzi TV
KATIBU wa Itikadi na Uenezi, wa Chama cha Mapinduzi CCM , Shaka Hamdu Shaka, amesema kupitia agizo la Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo la kumtaka atoe namba ya simu yake kwa wananchi kwa ajili ya kupokea kero na changamoto mbalimbali za wananchi tayari amepokea kero hizo za wananchi kwa njia mbalimbali za mtandao.
Amesema kwa takribani muda wa siku moja na masaa kadhaa amepokea ujumbe mfupi kwa njia ya kawaida jumbe 2974 za kero na changamoto na ujumbe wa njia ya WhatsApp amepokea jumbe 2664.
Akizungumza mkoani Dar es Salaam wakati wa mapokezi ya kumpokea Katibu Mkuu wa Chama hicho Taifa, Daniel Chongolo na Sekretarieti yake ya Halmashauri kuu, amesema jumbe hizo alizopokea zilizokuwa na viambatanisho na vielelezo vya kero mbalimbali za wananchi.
Shaka amesema hiyo inaashiria kwamba Sekretarieti hiyo na Chama chao wanayokazi yakufanya hivyo amehaidi kuanza kuzishughulikia huku akiwataka watendaji wa chama na serikali kuzifanyia kazi changamoto hizo, kila mmoja kwa nafasi yake atimize wajibu wake kwa nafasi yake.
"Nataka niwahakikishie watanzania kuwa Sekretarieti hii imebeb maono na imebeba mtazamo ipo tayari kutekeleza kwa vitendo adhima na nia ya Rais Samia Suluhu Hassan,"amesema na kuongeza,
"Tunakwenda kusimamia kero,changamoto, haki na dhuruma kuwahakilishia watanzania wanafikia mwisho wake kwani Rais Samia Suluhu Hassan aliwahi kusema Uongozi ni kuonyesha nia na sio kufunga njia,"amesema.
Amewataka viongozi wa Serikali walioteuliwa kufanya kazi kwa bidii kwani, wakati huu wanapaswa kujituma kuhakikisha kazi inaendelea.
By Mpekuzi
Post a Comment