PUMA ENERGY TANZANIA YAJITOSA KUHAMASISHA 'SPIDI 30' KWENYE MIKUSANYIKO YA WATU KUEPUKA AJALI |Shamteeblog.


Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania Domic Dhanh ( wa nne kulia waliosimama nyuma) akiwa na maofisa wengine wa kampuni hiyo, wadau wa usalama barabarani pamoja na wanafunzi ambao ni mabalozi wa usalama wakato wa kuadhimisha Wiki ya Usalama barabarani duniani iliyofanyika leo.




Matukio mbalimbali katika picha wakati wa kuadhimisha Wiki ya Usalama barabarani duniani ambapo wanafunzi ambao ni mabalozi wa usalama wameungana na Puma kutoa elimu kwa watumiaji wa vyombo vya moto na hasa kufuata na kuheshimu sheria ili kuepuka ajali.
Neema Swai( aliyevaa kofia wanne kutoka kulia) wa Shirika la Amend ambalo limejikita kutoa elimu ya usalama barabarani akiwa na wanafunzi ambao ni.mabalozi wa usalama wakitoa elimu kwa wateja wa liofika kujaza mafuta Kituo cha Puma Energy Tanzania.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania Dominic Dhanah akizungumza na waandishi wa habari kuhusu watumiaji wa vyombo vya moto barabarani.kuheshimu sheria za usalama barabarani sambamba na kuhamasisha spidi 30 maeneo ya mkusanyiko wa watu.
Sajenti Faustina Ndunguru kutoka Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani akizungumza kuhusu maadhimisho hayo huku akisisitiza madereva kuzingatia sheria ili kuepuka ajali.


 Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

KATIKA kuhakikisha kasi ya uchumi inaendelea kuimarika hususan kupitia shughuli za kiuchumi katika sekta ya usafirishaji kwa njia ya barabara, waendesha vyombo vya moto wametakiwa kuheshimu matumizi sahihi ya miundombinu hiyo na mipango mahususi inayoanzishwa kuepusha ajali za barabarani.

Miongoni mwa operesheni zinazosisitizwa kwa sasa ni kuzingatia mwendo wa ‘sipidi’ 30 katika maeneo mahususi yenye mikusanyiko ya watu wengi yakiwemo ya ibada, sokoni na maeneo ya shule.

Hayo yamesemwa na  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Puma Energy Tanzani Dominic Dhanah  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Usalama Barabarani Duniani iliyokuwa na kaulimbi ‘Love 30’ikiwa na maana ya kuhamasisha matumizi ya spidi 30 katika maeneo hayo.

“Barabara ni kichocheo muhimu kwa maendeleo ya kiuchumiu. Mwito wetu Puma Energy Tanzania kwa watumiaji wa barabara hususan madereva wa magari na wapanda pikipiki, ni kuhakikisha wanazingatia sheria za usalama barabarani na kwa muktadha wa kaulimbiu ya Love 30, kila mmoja aheshimu maeneo ya vivuko vya watembea kwa miguu,” amesema.

Ameongeza kampuni yake itaendelea kuwa mdau muhimu katika mapambano dhidi ya ajali za barabarani ili kunusuru maisha ya wananchi hususan wenye mahitaji maalumu wakiwemo wanafunzi.

Kwa upande wake Sajenti Faustina Ndunguru kutoka Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani Makao Makuu, amesema kwamba kuheshimu sheria za usalkama barabarani ni hatua muhimu ya kuepusha ajali.

“Katika hili nasi tunaungana na jumuiya ya kimataifa katika kaulimbiu ya ‘love 30’ kwa kuwa ni moja ya njia muhimu za kuepusha ajali.

Alisema endapo dereva au mwendesha pikipiki ataendesha kwa spidi ya 30, ni rahisi kuchukua hatua hata kufunga breki kwa haraka katika maeneo ya vivuko vya watembea kwa miguu.

Alisema kinyume chake, endapo dereva atapita akiwa na mwendo zaidi ya 30, ni vigumu kukabilana na ajali au changamoto yoyote ya dharura barabarani.

Wakati huo huo Meneja wa Shirika la Amend ambalo limekuwa likishirikiana bega kwa bega na wadau wengine wanaojitoa katika mapambano dhidi ya ajali za barabarani Simon Kalolo, amesema ni muhimu kwa watumiaji wa barabara hususan madereva, kuzingatia kaulimbiu ya ‘love 30’ kwa ajili ya kuokoa maisha watumiaji wengine wa barabara.

Kalolo amesema endapo kila mmoja atazingatia na kutekeleza sheria za usalama barabara, ajali za barabarani zitaendelkea kupungua na uchumi wan chi kupaa kwa maendeleo.

Aidha Mwanafunzi Moses Amon anayesoma darasa la sita katika Shule ya Msingi Bunge, Dar es Salaam, ambaye pia ni Balozi wa Usalama Barabarani wa Puma Energy Tanzania, aliwakumbusha madereva kutoa nafasi kwa wanafunzi pindi wanapowakuta wakisubiri kufanya hivyo kwenye vivuko vya waenda kwa miguu barabarani.

“Wanafunzi tumekuwa tukikumbana na changamoto ya ajali mara kwa mara ambazo wakati mwingine zinaweza kuepukika. Tunaomba madereva wawe sehemu ya kuepusha vifo na ulemavu kwetu wanafunzi,” alisema.

Naye Dereva Muthir Msellem Sheikha ameziomba mamlaka husika kuongeza alama za barabarani pale ambapo kuna ulazima wa kufanya hio, hususan kuwasaidia wenye mahitaji maalumu.

“Wakati mwingine katika maeneo ya kuvuka watembea kwa migguu, dereva uliye mbele unasimama ili kumpisha mwenye ulemavu au mwanafunzi aweze kupita, lakini dereva aliye nyuma hawezi kumwona kutokana na kimo chake na anaweza kuambua kuendelea na safari na madhara yake ni kumgonga mtembea kwa miguu.




By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post