Msajili wa Bodi ya maziwa nchini Dk. George Msalya amesema kuwa maadhimisho ya wiki ya maziwa ambapo Dunia huadhimisha siku hiyo kila Juni 1 na mwaka huu kitaifa yatafanyika jijini Tanga
Hayo ameyasema wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea madhimisho ya wiki ya maziwa duniani, amesema kuwa uagizaji maziwa kutoka nje ya nchi umekuwa ukiliumiza soko la ndani.
Amesema kuwa suala la unywaji maziwa kwa watanzania bado linaokena kutokua na hamasa licha ya serikali kutumia juhudi kubwa katika uhamasishaji wa matumizi ya maziwa
"Bado uelewa ni mdogo mtu badala ya kunywa maziwa wanakwenda baa kunywa pombe wakati maziwa ni muhimu kuliko hiyo pombe"amesema
Hata hivyo Dk.Msalya amewataka watanzania kuwa na uzalendo wa kutumia bidhaa za ndani za maziwa ili kuwainua wafugaji, wasindikaji na wachakataji wa bidhaa hiyo kwani zipo bidhaa nzuri za maziwa zinazotengenezwa nchini.
Dk.Msalya amesema kuwa nchi yetu bado ina uzalishaji mdogo wa maziwa kwani inazalisha Lita bilioni 3.4 ambapo ukigawanya kwa idadi ya watanzania, kila mtu atakunywa wastani wa Lita 50 tu kwa mwaka.
Amesisitiza kuwa mujibu wa wataalamu wa Afya mtu anatakiwa kunywa maziwa Lita 200 Kwa mwaka hivyo bado kuna uhitaji mkubwa wa uzalishaji zaidi wa maziwa kwani ni kinywaji muhimu Kwa Afya ya binadamu.
Aidha Dkt.Msalya amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa bodi hiyo mwaka 2005 Tanzania imepiga hatua katika uzalishaji wa maziwa kwani mwaka 2015 kushuka chini wastani kila mtu alikuwa anakunywa Lita 40 Hadi 45.
Hivyo kufikia mwaka 2015 hadi 2021 kila mtu anakunywa maziwa Lita 50 kwa mwaka ambapo katika pato la Taifa maziwa yanachangia kwa asilimia 30 huku katika sekta ya mifugo ikichangia Kwa asilimia 7.
Amesema kuwa maadhimisho hayo yatalenga katika kufanya tafiti kuhusu tasnia ya maziwa, kujifunza namna ya kufuga ng'ombe bora wa maziwa na kugawa maziwa katika makundi mahitaji kama wagonjwa katika hospitali mnalimbali.
Wiki ya Maziwa Duniani duniani ilianzishwa baada ya kugundua unywaji ni mdogo na sasa kuamua kuipigia chapuo ili kuyapa kipaumbele ili kuboresha afya za wananchi Kauli mbinunya mwaka huu ni ''Tunywe Maziwaa ya Kwetu,Uzalishaji na Usindikaji Kazi Iendelee''
Msajili wa Bodi ya maziwa nchini Dk. George Msalya,akizungumz na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitangaza maadhimisho ya wiki ya Maziwa kitaifa yatafanyika Mkoani Tanga.
By Mpekuzi
Post a Comment