TIMU YA WATUMISHI CHAMWINO YAWAFUNDISHA SOKA TIMU YA IRINGA VETERANI |Shamteeblog.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

Timu ya watumishi kutoka katika halmashauri ya Chamwino jijini dodoma week and hii imefanya ziara ya kimichezo mkoani Iringa na kucheza mechi ya mshikamano na timu mbili za veterans za mkoani Iringa

Timu hiyo ya watumishi Chamwino inayotoka katika Halmashauri ya Chamwino jijini Dodoma imeandaa mechi hizo za kirafiki kwa lengo la kucheza michezo ya kirafiki na timu za mpira wa miguu na volleyball za mkoani Iringa na kujenga mahusiano ya kirafiki na wachezaji wa timu hizo.

Timu hiyo ya watumishi wa chamwino ilianza kwa mechi iliyowakutanisha na timu ya Iringa Veteran ambapo hadi dakika tisini walikuwa wametoshana nguvu ya magoli mawili kwa mawili (2-2) mchezo uliopigwa majira ya asubuhi katika dimba la CCM Samora mkoani Iringa.

Katika mchezo huo timu ya Iringa Veterani ndio walikuwa wa kwanza kupata goli la kuongoza mwishoni mwa kipindi cha kwanza lililofungwa na Dr Idd ramadhani, hadi mapunziko walikuwa wanaogoza goli hilo moja licha ya kuzidiwa eneo la kiungo na kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo Dr. Idd Ramadhan aliwainua tena mashabiki kwa kuifungia timu yake goli la pili.

Kufuatia matoke hayo Timu ya Watumishi Chamwino walirudi mchezoni na kufanikiwa kurudisha goli zote mbili kupitia kwa mshambualiaji wao Costantine Rweyemamu katika kipindi cha pili.

Katika mchezo huo timu ya Watumishi Chamwino walioneka kuwa timu bora kwenye eneo la kiungo na kuwasumbua wapinzani ambao kwa kiasi kikubwa walilazimika kucheza mchezo wa kujihami zaidi ili kuondoa aibu ya uwanja wa nyumbani kufungwa na wageni hao.

Akizungumza mara baada ya mchezo nahodha wa timu ya Watumishi Chamwino Ally Komba alisema kuwa mchezo huo ulikuwa mzuri kwa pande zote mbili kwa sababu walicheza kwa kutoa burudani kwa mashabiki waliokuwa wamehudhulia mchezo huo.

Alisema kuwa wamekuwa Iringa kwa lengo la kucheza michezo mingi ya kirafiki na kuongeza marafiki wengine wapya ili kudumisha mshikamano kwa kuwa wamoja kwenye michezo na kufanya shughuli nyingine za kimaendeleo.

“Tumepokelewa vizuri Iringa na tumecheza mechi yetu ya kwanza huku tukiwa tunafurahia burudani ambayo tuliitegemea hapa,kwa kweli tumefurahia mazingira ya Iringa toka tumefika jana usiku hadi hii leo” alisema….

Kwa upande wake naohadha wa timu ya Iringa Veterani Kelvin Kalinga alisema kuwa mchezo ulikuwa mgumu na wenye ushindani mkubwa kutokana na timu zote mbili kuwa kwenye ubora uliosababisha timu hizo kufungana goli mbili kwa mbili.

Alisema kuwa lengo la mchezo huo ni kuongeza mshikamano baina wachezaji wa timu hizo ambao walikuwa hawafahamiani kwa kiasi kikubwa.

Naye mratibu wa timu ya Watumishi Chamwino Helen lisakafu alisema kuwa lengo la safari ya kutoka Halmashauri ya Chamwino hadi Iringa ni kudumisha umoja na ushirikiano baina ya wachezaji waliocheza zamani ambao wapo mikoa mingine.

Alisema kuwa wamekuwa wakitembelea mikoa mingi kwa lengo la kuongeza marafiki na kuongeza ushirikiano kwa wananchi na wachezaji wa timu ambazo wanaenda kucheza nazo. 




Kikosi cha timu ya Watumishi Chamwino ikiwa katika picha ya pamoja kwenye uwanja wa CCM Samora.

Mchezaji wa timu ya Watumishi Chamwino akitafuta namna ya kumtoka mchezaji wa timu ya Iringa Veteran

Mchezaji wa timu ya Watumishi Chamwino akitafuta namna ya kumtoka mchezaji wa timu ya Iringa Veteran.Timu ya Watumishi Chamwino ikiwa katika picha ya pamoja kwenye uwanja wa CCM Samora









By Mpekuzi

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post