Goddess of Rap Rosa Ree moja kati ya ndoto zake kubwa ni kuja kuwa mama na mwanamke mzuri kwa mwanaume wake ambaye Mungu atakuwa amempangia.
Rosa Ree amesema baadhi ya vigezo anavyovitaka kwa mwanaume wake ni kuwa 'smart' kujielewa, kumcha Mungu pia awe na akili.
"Ndoto kati ya ndoto zangu kubwa ni kuja kuwa mama na mke mzuri kwa mwanaume ambaye Mungu atanipangia, ambaye atakuwa smart, anayejielewa, ana akili na mcha Mungu"
"Ili kumpata mume wa aina hiyo inabidi mwenyewe ujielewe, huwezi kuwa wa aina fulani halafu ukampata mtu tofauti. Jinsi mtu utakavyojiweka ndiyo utapata mwanaume wa aina hiyohiyo" ameongeza Rosa Ree
Rosa Ree amesema hayo kupitia show ya Friday Night Live ya East Africa TV na East Africa Radio ambayo inaruka kila siku ya Ijumaa kuanzia 3:00 mpaka 5:00 usiku, pia huwa 'live' kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook, YouTube na Instagram ya East Africa TV.
from Author
Post a Comment